Vyeti vya  usajili vya kuendesha shughuli za sanaa alivyokabidhiwa leo.
Rapa Roma Mkatoliki,  akikabidhiwa cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mungereza, baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mungereza (kulia) akizungumza jambo.
Rapa Roma Mkatoliki akiwa katika ofisi ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

RAPA Roma Mkatoliki, leo Alhamisi amekabidhiwa cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ili aweze kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar, Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki aliwashukuru watu wote waliopaza sauti hadi kufutiwa adhabu hiyo, huku akiwaasa wasanii wenzake kuchukua hatua mapema za kujisajili.

Aidha Roma alisema kuwa, kitendo cha wimbo wake wa Kibamia ni sawa huku akivitaka vyombo vya habari kuacha kuupiga wimbo huo.