TANZANIA imetabiriwa kuwa moja miongoni mwa mataifa yanayokua kiuchumi Duniani, litakalotoa ushindani mkubwa katika soko la ajira kupitia watu wake, endapo mamlaka mbalimbali zinazohusika na taaluma zitaamua kuwekeza katika elimu ya ufundi stadi.

Hayo yalibainishwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafi ti ya REPOA, Dk Donald Mmari wakati wa kuhitimisha siku mbili ya warsha ya utafi ti wa 23 wa taasisi hiyo, iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya utafi ti na sera, kuelekea Tanzania ya Uchumi wa kati wa Viwanda 2025. Alisema kuna kila sababu ya mamlaka zinazohusika kuwekeza zaidi katika kutoa elimu ya ufundi stadi nchini ili kusaidia kupika wataalamu wa fani mbalimbali ambao mbali na kushiriki kufanya kazi zenye manufaa kwa nchi, lakini pia watakaosaidia kutoa ushindani katika soko la ajira la kimataifa. Katika mkutano huo, Dk Mmari alisema miaka iliyopita Tanzania ilikuwa na vyuo vingi vilivyokuwa vikitoa mafunzo ya ufundi, kabla ya miaka ya hivi karibuni vyuo hivyo kupandishwa hadhi na kuwa vyuo vikuu, ndiyo kwa kiasi kikubwa kumesababisha kufi fi a kwa wingi wa wataalamu waliokuwa wakizalishwa na vyuo hivyo.
“Nchi nyingi ambazo zimeendelea na zenye uwezo wa kuhimili ushindani kwenye soko la kimataifa, msingi wake mkubwa umetokana na uwekezaji walioufanya katika elimu, ujuzi hivyo kuzalisha wataalamu, ili kushindana nao ni lazima Tanzania nayo ikabadili mwelekeo wake kwa kuwaandaa vijana watakaokuwa na ujuzi,” alisema Dk Mmari. Aidha katika warsha hiyo iliyowahusisha pia wataalamu wa masuala ya uchumi kutoka nje ya nchi, Dk Mmari alibainisha uwepo wa changamoto ya uhaba wa wataalamu katika nyanja mbalimbali, hali aliyodai kuwa inasababishwa na kutokuwepo na uwekezaji huo kwa elimu ya ufundi stadi.
Alisema Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya vyema kwa kuzalisha wataalamu wa kutosha wa kufanya kazi katika viwanda vya ndani nan je ya nchi, endapo itaamua kurudi chini kuangali upya mfumo wake wa utoaji wa elimu, jambo litaloisaidia pia kufi kia malengo ya ujenzi wa viwanda na kuwa na bidhaa zenye ushindani katika soko la kimataifa. Aidha mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, Jacqueline Mkindi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya ‘Tanzania Horticultural Asspciation’ (TAHA), alisema warsha hiyo mbali na mambo mengi waliyojifunza, kwa kiasi kikubwa imewasaidia kubaini uratibu mzuri utakaosaidia kuwajengea uwezo vijana na hivyo kuondoa changamoto ya uhaba wa wataalamu katika fani mbalimbali nchini.