Tiko Hassan
KUFUATIA Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuliamsha dude la watu wanaowasainisha mikataba feki wasanii wa filamu, msaniii wa Bongo Muvi, Tiko Hassan amejikuta akiamka usingizini kwa kuwa na mwanasheria.

Akistorisha na Za Motomoto News, Tiko alisema kuwa Dk Mwakyembe alimwamsha usingizini kwani kwa sasa ana mwanasheria wake na pale anapotakiwa kuingia mkataba wowote wa kazi, lazima amshirikishe kwanza ili kukwepa kutapeliwa kama ilivyotokea kwa wasanii wenzake ambao wamefanya kazi nyingi za filamu, lakini wamejikuta wakitapeliwa haki zao.
“Unajua watu wamekuwa wakitumia nafasi ya njaa zetu kutudidimiza kwa kutusainisha mikataba ya ajabu hivyo nimeshtuka baada ya waziri wetu kuzungumza bungeni na kuchukua tahadhari mapema ambapo kwa sasa nina mwanasheria na meneja wangu hivyo siyo rahisi kuingia kwenye mikataba isiyoeleweka,” alisema Tiko. Hata hivyo, aliwataka wasanii wenzake kuwa makini na waepuke kukurupuka na kuingia mikataba isiyoeleweka na ikiwezekana wawe na wanasheria ili haki zao zisiendelee