Wavulana 12 waliookolewa katika pango lililojaa maji kaskazini mwa Thailand wiki iliopita wamezungumza hadharani kuhusu tukio hilo kwa mara ya kwanza wakitaja tukio hilo kuwa la miujiza wakati waogeleaji walipowapata.

Adul Sam-on ,14, mwanachama wa pekee wa kundi hilo ambaye anazungumza lugha ya kiingereza aliambia waandishi wa habari kwamba aliweza kusema ''hello'' pekee wakati waogeleaji wa Uingereza walipotokezea.
Wavulana hao walikuwa wamekwama katika pango la Tham Luang kwa takriban wiki moja. Waliondoka hospitalini siku ya Jumatano na sasa wanaelekea nyumbani.
Wavulana hao 12, ambao ni wananchama wa timu ndogo ya soka , kwa jina Wild Boars, walionekana katika mkutano na wanahabari wakiwa wamevalia jezi zao za soka katika eneo la Chiang Rai.
Walisalimiwa na bango lililosema ''Tunaikaribisha timu ya Wild Boars nyumbani'' katika jukwaa lililotengezwa kama uwanja wa soka
Vijana hao waliketi na wanachama wa jeshi la wanamaji wa Thai waliowaokoa
wavulana hao waliingia katika chumba cha mkutano na wanahabari wakiwa wamevalia jezi zao za kusakata sokaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionwavulana hao waliingia katika chumba cha mkutano na wanahabari wakiwa wamevalia jezi zao za kusakata soka
Mvulana mmoja alielezea vile walivyoishi katika maji ndani ya mawe ya pango hilo . 'Maji ni safi'' , alisema. ''Maji pekee hakuna chakula''
Chanin "Titan" Wibrunrungrueang, 11, alisema: "Nilijaribu kutofikiria kuhusu chakula kwa kuwa kingenifanya kuhisi njaa."
Presentational grey line

Walikuwa na moyo wa kutoshindwa

Ulikuwa mkutano mzuri na vyombo vya habari.
Mzaha wa kwanza ulitolewa na muogeleaji wa jeshi la wanamaji wa Thai alipojitambulisha: Jina langu ni Baitoey na mimi ndio mrembo zaidi katika pango.
Watu walicheka katika chumba hicho , wa kwanza kuzungumza alikuwa Adul , kijana aliyewasiliana na waogeleaji wa Uingereza.
Alisema kocha wake alimtaka kutafsiri .majibu yake: Tulia siwezi kuelewa haraka! watu wakazidi kucheka. Marafiki za wavulana hao na wauguzi kutoka hospitali ya Chiang Rai walikuwa wakitabasamu.
Na watu walipokuwa na hamu ya kutaka kujua vile walivyokwama , hali ndani ya chumba hicho ilibadilika na kila mtu akawa makini.
Vijana hao walinyamaza na kusikiza vile mkufunzi wao alivyosema kuhusu ubao uliowasaidia kuwa hai.
Wakati Titan, ambaye ni mdogo wa wote 12 aliposema hakutaka kufikiria kuhusu chakula kwa sababu kilimfanya kuhisi njaa , wengine walicheka kwa kelele- ikidhihirisha wazi kwamba licha ya hali mbaya waliokuwa nayo walikuwa na moyo wa kutoshindwa.
Presentational grey line
Wavulana hao walitoweka mwezi Juni 23 na wakapatikana na waogeleaji tarehe 2 Julai. Wanamaji wa Thai baadaye wakawaletea chakula.
Kundi hilo la vijana lilielezea vile lilivyoshirikiana na waokozi wao kwa zaidi ya juma moja, hadi walipookolewa. Tulicheza , Titan alisema. ''Baitoey aliibuka mshindi mara kwa mara na alikuwa mfalme wa pangoni''.
Waokoaji wa pango hilo wakifanya tambiko katika pango hilo
Kocha wa timu hiyo, Ekapol Chantawong, ambaye aliokolewa pamoja nao , alituma rambirambi kwa mwanajeshi Suman Kunan, ambaye alifariki wakati wa operesheni hiyo.
''Tunafurahi kwamba Saman alijitolea maisha yake kutuokoa ili tuishi maisha yetu. wakati tuliposikia habari hizo tulipata mshtuko'' , alisema.
''Tulikuwa na huzuni tulihisi kana kwamba tulileta huzuni katika familia yake''.
Baadhi ya wavulana walisema kwamba watajifunza katika tukio hilo .
Mmoja wao aliahidi kuwa mwangalifu ili kuweza kuishi zaidi. Mwengine alisema ''uzoefu huu ulinifunza kuwa na subra na nguvu''.
Vijana hao wanatarajiwa kutawazwa kuwa watawa wa budha kwa muda mfupi , utamaduni wa wanaume nchini Thailand ambao walikabiliwa na kisa kibaya

Je uokoaji ulifanyika vipi?

Wavulana hao na mkufunzi wao walikwama kabla ya mvua kuwazuia kutoka kupitia njia ya pango hilo la Tham Luang, ambapo walikuwa wamepanga kukaa kwa takriban saa moja.
wavulana hao walikuwa wakinywa maji pekeeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionwavulana hao walikuwa wakinywa maji pekee
Siku tisa zilipita kabla ya wavulana hao kupatikana na waogeleaji wawili wa Uingereza . haikujulikana mara ya kwanza ni vipi wangetolewa katika pango hilo.
Na huku mvua zaidi ikitarajiwa , jaribio hatari la kuwaokoa lilifanyika .
Waogeleaji wataalam waliwaongoza wavulana hao na mkufunzi wao kupitia katika giza na maeneo yaliojaa maji hadi juu kuelekea mlango wa pango hilo.
Kila mvulana aliandamana na muogeleaji ambaye pia alimbebea mtungi wake wa hewa.
Vijana hao walidungwa sindano za kuwalemaza ili kuwazuia kubabaika.
Wavulana hao na mkufunzi wao waliokolewa kwa awamu tatu katika siku tatu.
Wote 13 walihamishwa katika hospitali ya Chiang Rai ambapo walipata matibabu na usaidizi wa kisaikolojia.