Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling anataka kusaini mkataba mpya huko Old Trafford. Mchezaji huyo wa kimataifa mwenye miaka 28 wa England ana chini ya miezi 12 iliyobaki mkataba wake wa sasa kukamilika. (Star)

Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Mjerumani Mario Gotze, 26, ameshuriwa kujiunga na meneja wake wa zamaniaJurgen Klopp huko Liverpool. (Sky Sports)
Zinedine ZidaneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZinedine Zidane
David Beckham anafanya mazungumzo na mchezaji mwenzake wa zamania huko Real Madrid Zinedine Zidane kuhusu kukisimamia klabu yake ya Inter Miami katika ligi ya MLS. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema anahisi kuwa katika hali nzuri asilimia 200 licha ya kupumzishwa na meneja Maurizio Sarri kati kati ya wiki. Alirudi uwanjani akiwa kikosi cha kwanza wakati wa mechi iliyomalizika kwa sare siku ya Jumapili na West Ham. (Sky Sports)
Eden HazardHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEden Hazard
Kipa mwenye miaka 25 wa Besiktas Loris Karius -ambaye yuko kwa mkopo huko Liverpool anasema anapata motisha kutoka kwa kipa wa zamani wa Ujerumani Olivier Kahn. (Bild - in German)
Wachezaji wa Everton wanaamini wanafanya maandalizi mengi wanapojiandaa kwa mechi za Ligi ya Primia chini ya usimamizi wake Marco Silva. (Sun)
Marco SilvaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarco Silva
Mlinzi wa Arsenal Matteo Guendouzi, 19, anasema wachezaji wa zamani wa Gunners na Ufaransa Thierry Henry na Patrick Vieira walichangia akipende klabu hicho. (L'Equipe - in French)
Mabingwa wa Uhispania Real Madrid wametangaza mpanngo wa pauni milioni 500 kujenga upya uwanja wa Bernabeu. (Mail)
West Brom wanayaka kumleta mshambualiaji wa Hednesford Town Lewis Archer, 20, huko Hawthorns wakati wanalenga kupata kipawa kipya nje ya Ligi. (Express & Star)

Bora Kutoka Jumapili

Jack GrealishHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJack Grealish
Kiungo wa kati Jack Grealish, 22, anatarajiwa kukataa ofa ya Tottenham na kusaini mkataba zaidi na Aston Villa. (Express)
Mwenyekiti wa Juventus Andrea Agnelli anataka mabingwa hao wa Italia kumsaini wing'a wa Manchester City mjerumani Leroy Sane, 22. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa zamani wa LA Galaxy raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 36, amepewa ofa ya kurudi klabu yake ya utotoni ya Malmo. (Sun)
Zlatan IbrahimovicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZlatan Ibrahimovic
Manchester City wanatajiunga na Manchester United katika mbio za kumasaini kiungo wa kati mholanzi Frenkie de Jong, 21. (Mirror)
City pia wataka kumsani tena kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, ambaye alikuwa na muda mfupi huko Etihad kama kijana na ambaye anatarajiwa klabua hiyi ya Ufaransa msimu ujao. (Star)
Mshambuliaji wa Ajax raia wa Brazil David Neres, 21, amehusishwa na Tottenham na Roma. (De Telegraaf, via Calciomercato)
Maxwel CornetHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaxwel Cornet
Fulham wanatarajiwa kutoa ofa ya pauni milioni 18 kwa mshambuliaji wa Lyon raia wa Ivory Coast Maxwel Cornet, 21. (Sun on Sunday)
Arsenal walikataa fursa ya kumsaini mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, 27, akiwa huko Cletic kwa sababu mholanzi huyo alikuwa mtulivu sana. (Bein Sports, via Metro)
Mlinzi wa Manchester City Kyle Walker, 28, anasema anataka kurudi nafasi yake ya beki na England baada ya kucheza kama kiungo cha kati na nyuma wakati wa kombe la dunia. (Mail on Sunday)