Mahakama ya kijeshi imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kutokana na ghasia ambapo mwandishi wa habari aliuawa na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu kubakwa.

Mahakama imeiamrisha serikali ya Sudan Kusini kumlipa kila muathiriwa wa ubakaji dola 4,000 kama fidia.
Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa katika hoteli ya Terrain kwenye mji mkuu Juba mwaka 2016.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliwalaumu walinda amani kwa kushindwa kuitikia msaada wa waathiriwa.
Wanajeshi wa Sudan Kusini wamelaumiwa kwa kuendesha uhalifu mara kadhaa tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 lakini hili ndilo lilikuwa shambulizi baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni.
Hii ndiyi mara ya kwanza wanajeshi wameshukiwa kwa kuendesha uovu Sudan Kusini, taifa janga zaidi duniani ambalo lilipata uhusu wake mwaka 2011.

Kipi kilifanyaika mahakamani?

Mahakama iliiamrisha serikali iilipe familia ya mwandishi wa habari John Gatluak ngombe 51 kama fidia.
Alikuwa akichukua hifadhi kwenye hoteli hiyo wakati aliuawa.
A South Sudanese soldier is checked as he arrives for sentencing over the rape of foreign aid workers and the murder of a local journalist in an assault on the Terrain Hotel in the capital Juba in 2016 at a military court in Juba, South Sudan, September 6, 2018.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwanajeshi akikaguliwa alipowasili kuhukmiwa
Wanajeshi wawili walipatikana na hatia ya kumuua na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Wengine watatu walipatikana na hatia ya kuwabaka wafanyakazi wa kuto misaada, wanne kwa dhuluma za kingono na mwingine kwa wizi wa kutumia nguvu.
Walihukumiwa kati ya vifungo vya miaka 7 na 14 jela.
Shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mapigano makubwa mjini Juba kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi.
Zaidi ya watu 70 wakiwemo wakiwemo walinda amani wawili wa Umoja wa Mataifa waliuawa wakati wa mapigano ya siku tatu.
A South Sudanese military officer is seen before the hearing of 10 soldiers sentenced over the rape of foreign aid workers and the murder of a local journalist in an assault on the Terrain Hotel in the capital Juba in 2016, at a military court in Juba, South Sudan, September 6, 2018Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMahakama ya jeshi ilifurika wakati hukumu hizo zilitolewa
Watoa misaada wa kigeni walibakwa wakati wanajeshi walivamia hoteli hiyo.

Watu wamesema nini kuhusu hukumu hizo?

Wakili aliyewakilisha waathiriwa wa ubakaji Issa Muzamil Sebit alisema wateja wake hawakuridhishwa na hukumu hiyo.
Fidia waliyopata ilikuwa ya aibu, aliongeza.
Naye wakili wa washtakiwa Peter Maluang Deng alisema alishangazwa na hukumu hiyo akisema atakata rufaa.
Hata hivyo Amnesty International imekaribisha hukumu hizo.

Kesi hii ina maana gani

Serikali ya Afrika Kusini itatumia fursa hii kudai kuwa inapambana na dhuluma zilizofanywa na wanajeshi.
Lakini hiki kilikuwa ni kesi cha kiwango cha juu ni nadra kuona wanajeshi wakiletwa mbele ya hukumu kwa dhuluma walizotendea raia wa kawaida.
Jeshi katika pande zote mbili za mzozo zinaonekana kuwa na wakati mgumu kudhibiti wanajesi wao.
Umoja wa Mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu yamewalaumu kwa kuendesha uhalifu wa kvita
Mwaka 2015 Muungano wa Afrika ulitoa wito wa kubuniwa kwa mahaka,a maalum kuwahukumu washukiwa wa uhalifu wa kivita. Lakini hilo bado halijafanyika.