Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watu
walionusurika  katika  ajali ya kivuko cha MV Nyerere wakati
alipotembelea Kituo cha Afya cha Bwisya  kisiwani humo Septemba 24,
2018. Wengine ni mwananchi ambao bado wamepotelewa na  ndugu na jamaa
katika ajali hiyo wakisubiri kutambua miili endapo itaonekana.

Gari la wagonjwa  likiwa limeegeshwa kwenye jengo la Kituo cha Afya cha
Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani  Ukererwe ili kuteremsha mwili
wa mtoto  ambao waokoaji  waliupata katika kivuko cha MV Nyerere
Septemba  24, 2018. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kituo hicho
leo asubuhi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akikabidhi  kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isaack Kamwelwe mchango wa sh.
milioni 10 zilizotolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia katika  ajali ya
Kivuko cha MV Nyerere  kilichozama ktika kisiwa cha Ukara wilayaniu
Ukerewe, Septemba 20, 2018.  Makabidhiano hayo yalifanyika  katika
kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara, Septemba 24, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali, Venance Mabeyo  baada ya kumkabidhi jukumu kuwa msimamizi mkuu
wa operesheni ya uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye
kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 24,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu,
Jenista Mhagama (katikati)  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Profesa Faustine Kamuzora kwenye kijijii cha Bwisya katika kisiwa cha
Ukara wilayani Ukerewe baada ya Waziri Mkuu kutembelea eneo kilipozama
kivuko cha  MV Nyerere kijijini hapo Septemba 24, 2018.