Kajala Masanja
 STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja amewapa somo mastaa wenzake kuwa washtuke mapema katika kila jambo wanalolifanya na kwamba, zama za kula bata zimepitwa na wakati.Akizungumza na Risasi Jumamosi, Kajala alisema yeye kuna wakati alijisahau na kujikita kwenye mambo hayo lakini sasa ameshtuka na ndio maana hawezi kuonekana viwanja ‘akitumbua’ pesa.

“Unajua huu ni wakati wa mastaa kushituka na kufanya mambo yatayowasaidia wao na familia zao siku za baadaye. Mimi nimestuka, niliyokuwa nayafanya siyo mazuri ila sasa nafanya yale ambayo mtu makini anatakiwa kuyafanya.” Alisema Kajala. Kajala mbali na kufanya sanaa ya uigizaji, anatangaza kipindi cha bahati nasibu kwenye TV na pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment.