Beki Mhispania Marcos Alonso, 27, amesaini mkataba mpya na Chelsea ambao utadumu hadi Juni 2023. (ESPN)
Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 25, anasema hana nia ya kuondoka klabu ya Serie A. (AS)
Kumfuta meneja Julen Lopetegui, 52, kunaweza kuigharimu Real Madrid euro milioni 18. (Sport)

Julen LopeteguiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJulen Lopetegui
Lopetegui atafutwa na meneja wa akiba Santiago Solari, 42, achukue mahala pake kabla ya mechi ya Jumapili ya El Clasico dhidi ya Barcelona. (Star)
Aliyekuwa kocha wa Uhuspania Lopetegui bado atasimamia El Clasico. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mlinzi wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 29 amefichua kuwa atakuwa tayari kujiunga tena na klabu ya zamani Ajax siku za usoni. (Sky Sports via De Telegraaf)
Victor MosesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVictor Moses
Wing'a raia wa Nigeria Victor Moses, 27, yuko tayari kuondoka Chelsea huku akiwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza chini ya umeneja wa Maurizio Sarri. (Goal)
Meneja wa Atlanta United Gerardo Martino, ambaye ametangaza kuwa ataondoka mwishoni wa msimu wa MLS akiwa njiani kuwa meneja mpya wa Mexico. (CBS)
Nyota wa zamani wa Barcelona Xavi anasema hawezi kufunza timu kucheza kama timu zinazosimamiwana Jose Mourinho. (FourFourTwo)
XaviHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionXavi
Kocha wa Togo Claude Le Roy amemuunga mkono mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane 26, kuhamia klabu ya Manchester United. ((Star)
Mmiliki wa klabu ya Nottingham Forest Evangelos Marinakis alisafiri kutoka Athens kupeleka ujumbe kuwa matokeo yao ni lazima yaimarike baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza katika mechi saba. (Mail)

Bora Zaidi Kutoka Jumanne

Antonio ConteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntonio Conte
Antonio Conte yuko juu zaidi ya orodha ya Real Madrid kuwa meneja wao mpya ikiwa watamfuta Julen Lopetegui, lakini hilo litafikisha kikomo fursa ya kumsaini Eden Hazard ambaye alikuwa na uhusiano mbaya na Muitalia huyo huko Chelsea. (Mirror)
Kocha wa Chelsea Marco Ianni, anayechukuliwa hatua na FA kwa kuhusika katika mzozo ya kuvuka mstari wakati upande wake ulitoka sare ya 2-2 na Manchester United, huenda akachukuliwa hatua zaidi baada ya kuibuka kuwa hata hakustahili kuwa katika eneo la kiufundi. (Mail)
Mchezaji wa Liverpool Divock Origi huenda akahamia Uturuki huku vilabu vya Besiktas na Fenerbace vikitaka kumsaini mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Ubelgiji. (Fanatik, via Talksport)
Divock OrigiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDivock Origi
Fulham wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya mkataba na mlinzi mwenye miaka 18 Ryan Sessegnon, ambaye amekuwa akilengwa sana na Tottenham, ambaye amebaki na miezi 18 mkataba wake wa sasa kukamilika. (Mail)
Mlinzi wa Inter Milan raia wa Slovakia Milan Skriniar, 23, ambaye amehusishwa na Manchester United na Manchester City, bado hajakubaliana na mkataba mpya na klabu hiyo ya Italia. (Calciomercato)
Chelsea watafikiria kumsaini mchezaji wa Genoa mshambuliajia raia wa Poland Krzysztof Piatek, 23, mwezi Januari. (Mail)