Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki akizungumza na Waandishi jana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ikiwa ni matayarisho ya kusherehekea miaka 73 ya Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 24
Oktoba husherehekewa Duniani kote na kwa Tanzania yataadhimishwa jijini
Dar es Salaam na Zanzibar, kushoto ni Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi
wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na kulia Bw. Deusdedit B. Kaganda
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.

Bw.
Deusdedit B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano  wa
Kimataifa kulia akimkaribisha Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kushoto kuzungumza na waandishi wa
habari katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Mkutano huo ulifanyika
kufuatia tarehe 24 Oktoba, Umoja wa Mataifa utaadhimisha Miaka 73 ya
tokea kuanzishwa kwake. Katikati Mhe. Dkt. Damas Ndumaro (Mb) Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Bw.Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania
aliyekaa kushoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere akilelezea juu ya
maendeleo ya Umoja huo na kaulimbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku
ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba iliyobeba ujumbe wa "Uwezeshaji
Vijana na Ubunifu kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu" 

Baadhi wa waandishi wa Habari walioshiriki katika mkutano wa Waandishi wa  Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.