Mwenyekiti wa Enzi Foundation Bi Rehema Simkoko akielezea historia fupi na malengo ya taasisi yake kwa wageni waalikwa waliohudhuria ukumbini hapo jana katika jiji la Den Haag nchini Uholanzi. |
Mwenyekiti wa Enzi Foundation Bi.Rehema Simkoko akimtunuku tuzo ya kumuenzi Mzee Hamidu, mmoja wa wazee wenye Upendo na waendelezaje bora wa Mila na tamaduni zetu nje ya nchi. |
Mwanamuziki kutoka nchini Angola anakwenda ka jina Alzira Assis akitumbuiza kwenye usiku wa Mtanzania huku wageni waalikwa wakiwa makini kumsikiliza jinsi anavyoburudisha |
Wageni waalikwa kutoka nchini mbalimbali wakifuatilia usiku wa Mtanzania hapo jana |
Mmoja wa wanamitindo akipita mbele ya wageni waalikwa kwenye usiku wa Mtanzania na vazi la kitenge lililobuniwa na mwanadada Bahia Kihondo wa Holland Fashion. |
Kiukweli Usiku wa Mtanzania ulipendeza kwa mavazi mbalimbali yaliyobuniwa na Holland Fashion |
Wageni waalikwa wakipiga makofi kuupongeza uongozi wa Enzi Foundation |
Wageni waalikwa wakifuatilia mambo yanayojiri usiku wa Mtanzania ulioandaliwa na Enzi Foundation |
Usiku wa Mtanzania ulipendeza kihivii...Full vitenge mpaka raha Gebo Family |
Wageni kutoka Ubelgiji ambao nao walihudhuria usiku wa Mtanzania nchini Uholanzi |
Burudani ya mziki ikitumbuizwa na mwanadada kutoka nchini Angalo kwa jina la Alzira Assis huku wanamitindo wakipita na mavazi ya Kanga. |
Burudani ya muziki ilichukua nafasi na watu wakaselebuka |
Dj Andrew wa nchini Uholanzi akiwa na Dj Jamal kutoka Ubelgiji wakia kazini kuhakikisha |
Mrembo wa miaka yote mwanamama Sexy mama katika ubora wake ndani ya usiku wa Mtanzania |
Huku burudani zikiendelea watu walikuwa makini kuhakikisha hawapitwi na kila kinachoendelea jukwaani ndani ya usiku wa Mtanzania. |
Usiku wa Mtanzania na mavazi ya kitanzania,hapa wageni waalikwa wakifurahia baadhi ya mambo ukumbuni |
Vazi la kanga likitawala jukwaa |
Moja ya ubunifu wa Holland Fashion |
Wanamitindo wakiwa jukwaani kuonyesha mavazi yaliyobuniwa na mwanamitindo Bahia Kihondo wa Holland Fashion.{Picha zote na Maganga One Blog} |
Mwanamuziki Alzira kutoka Angola akiendelea kutumbuiza katika usiku a Mtanzania nchini Uholanzi |
Vazi la kanga likichukua nafasi yake |
Wanamitindo wakiwa katika vazi la kanga |
Mavazi ya asili ya Kimasai nayo yalileta raha yake katika kuyaangalia jukwaani |
Mc wa jana alikuwa ni ndugu Abeka kutoka Radio Africa Europe ambaye aliupamba vyema usiku wa Mtanzania |
Kitenge au kanga ubunifu huu wote utaupata kutoka Holland Fashion chini ya mbunifu wa mavazi B.Bahia Kihondo ambaye anapatikana kwa njia ya isntagram @hollandfashion |
Mwenyekiti na muhasisi wa Enzi Foundation Bi.Rehema Simkoko akisakata nyimbo za kale ndani ya usiku wa Mtanzania |
Kijana mdogo ambaye alikuwa akishangiliwa kila anapopita jukwaani kwa jinsi alivyokuwa anapendeza na mavazi yote aliyopita nayo |
DUMISHENI UPENDO,AMANI,UTULIVU NA UMOJA ni moja kati ya maneno ambayo yataenziwa siku zote na baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. |
0 Comments