Derartu Tulu,mwanamke wa kwanza mweusi wa Kiafrika kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki,na sasa ameteuliwa kuwa rais wa Shirikisho la riadha la Wanawake nchini Ethiopia,.
Anaichukua nafasi ya mwanariadha nguli Haile Gebrselassie.

Kujiuzulu kwa Haile Gebrselassie bila kutarajia mwanzoni mwa wiki hii kumejiri baada ya maandamano yaliyokuwa yakishutumu vifaa duni vya mafunzo katika mkoa wa Oromia, mahali ambako kunatajwa kuwa makao ya wana riadha nguli kutoka nchini Ethiopia .
Alikuwa akisisitiza kwa nguvu zake zote juu ya kampeni ya miaka miwili iliyopita kuleta mabadiliko,akisema shirikisho la riadha nchini humo linapaswa kuruhusiwa kuongozwa na watu wenye kaliba ya michezo.
Lakini hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa nafasi yake ya urais ilikuwa inadharauliwa , na hivyo kumzuia kutekeleza baadhi ya sheria na kanuni za shirikisho.
Haile Gebrselassie ajiuzulu urais wa riadha na kuteuliwa Derartu Tului kushika wadhifa huoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNguli wa riadha nchini Ethiopia Haile Gebrselassie.
Rais wa Shirikisho la wanariadha wa jamii ya Oromia, Dagnachew Shiferaw, ameiambia BBC kwamba Haile hakuweza kukidhi haja kwa kile alichoahidi wakati alipokuwa akishika mamlaka.Na wanariadha wamekuwa wakihoji juu ya hali hiyo ..Jamii nyingine ya wanariadha wana wasiwasi kwa kujiuzulu kwake na kudai kuwa kutazorotesha tasnia ya wanariadha nchini Ethiopia.
Mbobevu wa masuala ya riadha nchini humo ameiambia BBC kuwa, 'Wakati mashindano makubwa kama vile michuano ya riadha ya Doha na ile ya limpiki iko mbele yao, kujiuzuru kwa Haile kunaweza kuleta hasara kubwa.
Haile alimteua Derartu kama nafasi yake Haile alimteua Derartu kushika nafasi yake na kamati ya shirikisho ilimteua kuwa rais wa mpito mpaka hapo mkutano wa dharula utakapoitishwa katika miezi ijayo.