Morocco imezindua treni inayokwenda kwa kasi zaidi barani Afrika - itakayopunguza nusu ya muda unaotumika kusafiri katika miji ya kibiashara na kiviwanda Casablanca na Tangi
Mfalme Mohammed VI na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron waliipanda treni hiyo katika safari ya uzinduzi kutoka Tangier hadi katika mji mkuu Rabat.

treniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Ufaransa Eammanuel Macron amealikwa katika uzinduzi wa treni ya kasi Morocco
treniHaki miliki ya pichaREUTERS

Takwimu kuu kuhusu treni ya kasi Afrika:

  • Treni imepangiwa kwenda kwa kasi ya 320km kwa saa
  • Itakapunguza kwa zaidi ya nusu muda unaotumika kusafiri 200km kutoka mji wa Casablanca hadi Tangi kuwa safari ya saa mbili.
  • Inakwenda kwa kasi ya mara mbili zaidi kuliko treni ya mwendo kasi ya Afrika kusini inayouunganisha uwanja wa kimataifa wa ndege Johannesburg hadi katika mji wa kibiashara wa Sandton
  • Inagharimu 22.9 billion dirhams ($2.4bn; £1.8bn), kwa mujibu wa shirika la habari la kitaifa MAP
  • Ilichukua miaka saba kuijenga reli ya treni hiyo.
Afrika inatazamia kuimarisha miundo mbinu ya usafiri kushinikiza biashara, uwiano na utangamano wa kieneo.
Mataifa ya Afrika yanakumbatia mfumo wa reli ya mwendo kasi katika kujaribu kushinikiza na kukuza uchumi na kuimarisha kasi za kusafirisha bidhaa baina ya mataifa kibiashara.
Katika miaka 20 iliyopita jitihada za kufufu mfumo wa reli umechangi baadhiya maatifa kuamua kubinafsisha huduma hizo hususan katika mataifa ya magharibi na mashariki ya Afrika.
Reli ya kisasa ya SGR nchini KenyaHaki miliki ya pichaMICHAEL KATEL
Image captionReli ya kisasa ya SGR nchini Kenya

Kenya:

Mradi wa reli mpya ya kisasa nchini Kenya SGR umefadhiliwa na serikali ya China ambao unaunganisha mji wa pwani wa Mombasa na Nairobi ulifadhiliwa kwa mkopo wa kima cha $3bn kutoka kwa benki ya China ya Exim katika kipindi cha miaka 15.
Reli hiyo ya SGR ni miongoni mwa miradi muhimu ilioahidiwa na rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wake, ukizinduliwa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa urais uliopita.
Awamu ya kwanza ya reli Kenya ilianza kazi mnamo Juni 2017.
Kenya sgr

Tanzania:

Jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge liliwekwa na rais John Pombe Magufuli mnamo Aprili 2017.
Mradi huo umenuiwa baadae kuziunganisha nchi za Rwanda na Burundi pia.
Katika awamu hii ya kwanza, ujenzi utakuwa wa reli yenye urefu wa kilomita takribani 300, ambayo itatoka jijini Dar es Salaam na kuishia mkoa wa jirani wa Morogoro.
Ni reli ya kisasa, na ya kwanza Afrika Mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nguvu ya umeme.
Reli hiyo inajengwa kwa awamu ya kwanza na kampuni kutoka nchi mbili, Uturuki na Ureno kwa gharama ya takriban dola bilioni 1.2 za Kimarekani.
Dkt Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionDkt Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Ethiopia

Reli mpya ya aina yake inayounganisha mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na mji mkuu wa Djibouti imezinduliwa Oktoba 2016.
Reli hiyo mpya ina urefu wa kilomita 752 na inatoka Addis Ababa hadi bandari ya Doraleh katika mji wa Djibouti, kwenye ghuba ya Aden.
Inasafirisha abiria na mizigo.
Sehemu kubwa ya reli hiyo imo Ethiopia, Kilomita 652 kutoka Addis Ababa hadi Dewale mpakani, na sehemu iliyosalia Djibouti.
Reli hiyo inaunganisha Addis Ababa na mji wa Djibouti
Image captionReli hiyo inaunganisha Addis Ababa na mji wa Djibouti
Gharama ya ujenzi wa reli hiyo ni dola 4 bilioni za Marekani. Ufadhili umetoka kwa benki ya serikali ya China ya Exim & Import (70%) na sehemu iliyosalia kutoka kwa serikali ya Ethiopia.
Benki ya maendeleo ya Afrika inataja kwamba katika ubinfasishaji ufadhili bora, muongozo wa sheria na utaalamu ni mambo muhimu.
Mradi wa mtandao wa reli za kasi Afrika, ni sehemu ya ajenda ya Umoja wa Afrika 2063 na umenuia kuimarisha mifumo iliyopo sasa ya kitaifa ya reli.