Aliyekuwa wakati mmoja kiongozi wa kundi la wahalifu ambaye aliandika kitabu kuhusu jinsi aliishi maisha yake, ameuawa kwa kupigwa risasi siku moja kabla ya kutolewa kitabu chake.
Nedim Yasar, 31, alipigwa rasasi wakati akitoka kuzindua kitabu hicho siku ya Jumatatu kwenye mji mkuu wa Copenhagen.

Yasar alipelekwa hospitalini lakini akafariki kutokana na majeraha. Kitabu chake kilichapishwa siku ya Jumanne.
Awali alikuwa amesema kulikuwa na njama ya kumuua mwaka uliopita.
Katika kisa hicho cha siku ya Jumatatu mtu ambaye alikuwa amevaa vazi leusi alimfyatulia Yasar takriban risasi mbili kwa mujibu wa polisi wa Copenhagen.
Police in Copenhagen, Denmark, at the scene of the shooting of former gang leader Nedim Yasar, 20 November 2018Haki miliki ya pichaEPA
Image captionEneo la mkasa mjini Copenhagen
Yasar, ambaye alizaliwa nchini Uturuki na kuwasili Denmark akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa kiongozi wa genge la wahalifu la mjini Copenhagen Los Guerreros, kundi sugu lennye uhusiano na biashara ya dawa za kulevya kwa mujibu wa polisi.
Alihama genge hilo mwaka 2012 na kujiunga kwenye mpango wa kubadili tabia baada ya kugundua kuwa angekuwa baba kulingana na shirika la habari la Ritzau.
A book entitled "Roots - a gangster's way out" by author Marie-Louise Toksvig about the life of Nedim Yasar, 20 November 2018Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKitabu cha Yasar kilitolewa Jumanne
Kisha akawa mshauri wa vijana na kujitengenezea jina kwa kuandaa kipindi kwenye kituo cha radio cha Radio24syv.
Kufuatia kufichuka taarifa za kuuliwa kwa Yasar Radio hiyo ilichapisha picha ya ofisi yake ikiwa bendera ya Denmark ikiwa nusu mlingoti.
Kitabu cha Yasar, Roots: Kujitoa maisha ya ujambazia, kimendikwa na Marie-Louise Toksvig na kinaelezea safari ya Yasar anapojitoa kutoka maisha ya uhalifu.
Waziri wa sheria nchini Denmark, Søren Pape Poulsen, alitaja kifo cha Yasar siku Jumanne kama hususni na kitu kisicho na maana yoyote.