Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakitazama ajali ya kuanguka kwa mabehewa ya treni leo asubuhi.

TRENI inayotoa huduma za usafiri kati ya Stesheni ya Dar es Salaam na Pugu Stesheni imepata ajali leo Novemba 2,2018 eneo  la Karakata baada ya behewa mbili kuanguka.

Kwa mujibu baadhi ya abiria waliokuwa kwenye treni hiyo wamesema ajali hiyo imetokea leo kwenye saa moja kasoro asubuhi ambapo baada ya kufika eneo hilo mabehewa mawili yalipinduka.

Mmoja wa abiria hao aliyejitambulisha kwa  jina la Juma Jebe amesema yeye alikuwa behewa la nne kutoka mabehewa yaliyoanguka na kwamba baada ya tukio hilo kuna baadhi ya abiria walionekana kuzimia kutokana na hofu. Hata hivyo amesema anashukuru kwani hakushuhudia mtu yoyote kuumia.