Rais Mstaafu  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza mara baada ya kutunukiwa Tuzo  ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.



 Rais Mstaafu  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitunikiwa Tuzo  ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika tarehe 2-3 Novemba, 2018 jijini Windhoek ambao ulijadili "Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika".

Windhoek, Namibia


Rais Mstaafu  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo  ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.


Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika tarehe 2-3 Novemba, 2018 jijini Windhoek ambao ulijadili "Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika".


 Rais Mstaafu Kikwete ameishukuru WAELE kwa tuzo hiyo na kwa kutambua mchango wake katika kusukuma agenda ya ushiriki wa wanawake katika uongozi. Amesema kuwa, hakufanya hivyo kwa kutegemea kupata tuzo siku moja, bali alitimiza wajibu wake wa uongozi wa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi za uongozi kwa kuwa ni haki yao na sio fadhila. Amewashukuru wanawake aliowateua kaika uongozi kwa kutomuangusha katika madaraka aliyowapa.