Raia wa Madagascar leo wanapiga kura kuchagua Rais mpya.
Kampeni za uchaguzi nchini humo zilijawa na utata kufuatia matumizi ya fedha ya wagombea wakuu watatu kati ya 36 wanao wania nafasi hiyo.

Wagombea hao watatu, wanawania nafasi hiyo ambayo waliwahi kuishikilia hapo awali.
Rais anayemaliza muda wake Henry Rajaonarimampianina anawania pia tena awamu ya pili madarakani
Kampeni zake zimegubikwa na heka heka za kutaka kurudi tena madarakani kwa viongozi wenye nguvu ya kisiasa waliowahi kuitawala nchi hiyo Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.
Ravalomanana aliitawala nchi hiyo kuanzia mwaka 2002 hadi 2009 alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi yaliyofanywa na Andry Rajoelina, ambaye wakati huo alikuwa Meya katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo.
Viongozi wote hao walipigwa marufuku kuwania kiti hicho tenamwaka 2013 kufuatia shinikizo kutoka jumuia ya kimataifa, lakini sasa wamerudi tena kupambania kazi yao ya zamani.
Marais hao wa zamani wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwashawishi wapiga kura.
Wamekuwa wakipiga kampeni nchi nzima kwa kutumia Helikopta, wakisambaza fulana katika mikutano yao pamoja na kutoa matangazo katika vyombo vya habari vya taifa.
Kwa wagombea wadogo wa nafasi hiyo hawana uwezo wa kufanya hivyo ama kushindana nao.
Didier Ratsiraka ni miongoni mwa walio wahi kuongoza Madagascar kwa kipindi kirefuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDidier Ratsiraka ni miongoni mwa walio wahi kuongoza Madagascar kwa kipindi kirefu
Wapiga kura nchini humo wana matumaini kwamba Rais wao mpya atasaidia kupunguza umasikini, ghasia za kisiasa na pia tuhuma za rushwa serikalini.
Iwapo katika uchaguzi wa leo hakuta patikana mshindi uchaguzi wa awamu ya pili utafanyika tena Novemba mwaka huu.