Wema Sepetu na Aunt Ezekiel
STAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa pamoja na mambo mengi ambayo yamekuwa yakimtokea, rafiki yake wa kweli ni  Aunt Ezekiel kwani hajawahi kumchoka na kumtenga kama wafanyavyo wengine.
Akizungumza na Chanzo cha habari hiziWema alisema kuwa ana marafiki wengi lakini baadhi ni wanafiki ila Aunt ana upendo wa kweli kwake. “Nimegundua kuwa rafiki wa kweli kwangu ni Aunt, amenipa faraja ya kweli kipindi chote cha matatizo, naamini ana upendo na mimi,”alisema Wema.