NI siku nyingine tena tunakutana katika safu hii ya My Style ambayo inazungumzia mastaa mbalimbali na kueleza maisha yao ya kila siku yanavyoenda.
Leo tunaye staa mwenye viwango vyake kutoka Bongo Muvi, Kajala Masanja ambaye pia anamiliki kampuni yake ya filamu, Kay Entertainment. Hadi sasa ameshacheza filamu nyingi ambazo zimempa chati mbalimbali kama Devil Kingdom ya Kanumba, Sikitu, Fundi Seremala, Laana, Pishu na Mbwa Mwitu.
Katika safu yetu hii, Kajala ataweka wazi style yake ya maisha ya kila siku kuanzia mtoko hadi manukato kama alivyokuwa akihojiana na My Style.
My Style: Msomaji angependa kufahamu kwanza ni kitu gani unapenda kwenye maisha yako ya kila siku?
Kajala: Napenda sana kutuliza akili yangu wakati wote, napenda kukaa sehemu ambayo haina vurugu kwa sababu mimi mwenyewe sipendi kabisa purukushani na mtu yeyote yule.
My Style: Marafiki zako ni wa aina gani au unapenda wawe na tabia gani?
Kajala: Kwanza kabisa mimi kama Kajala huwa sina urafiki wa ndani kabisa kama ilivyo kwa wengine ila napenda tu kampani ya kawaida tukimaliza kila mtu ana zake lakini pia napenda kuzungukwa na watu wanaojielewa, wanaoweza kunifanya nikacheka kila wakati.
My Style: Una muda wa kukaa jikoni na kupika?
Kajala: Ninaweza lakini nina msaidizi ambaye anafanya hivyo kwa sababu ya kazi zangu za kila siku lakini kama naingia jikoni natoa kitu kizuri.
My Style: Vipi kuhusu upande wa kutoka unaweza ukatupia mwilini kama shilingi ngapi?
Kajala: Kwa kweli napenda sana kupendeza, wakati wowote hivyo kama mtoko ule ambao nimeupangilia kumaliza milioni ni kitu kidogo kuanzia begi, nguo na nywele.
My Style: Unatumia manukato gani, maana watu wengi wanasema unanukiaga sana.
Kajala: Nachanganya sana sana! Ila nikitoka siwezi kukosa kujipulizia Olympia, Tom Ford, Jadore na Scandal yaani nachanganya napata harufu nzuri sana.
My Style: Vipi maisha yako wewe na Paula?
Kajala: Ni marafiki sana, lakini kuna wakati navaa umama nakuwa mbogo mwisho wa siku kila mmoja akikaa mbali na mwe-nzake tuna-kumbu-kana.
My Style: Unapenda kufanya mazoezi na unapendelea kufanya muda gani?
Kajala: Mazoezi ni kitu ambacho naweza kusema kipo kwenye damu yangu. Napendelea sana kwenda kufanya asubuhi maana nikimaliza nafanya mambo yangu jioni kama siku za wikiendi.
My Style: Unapendelea wageni wa aina gani nyumbani kwako?
Kajala: Mgeni yeyote napenda ila awe mstarabu tu maana kwangu naona kama mgeni ni Baraka.
My Style: Nguo mpya huwa unanunua baada ya muda gani?
Kajala: Kwanza kurudia nguo inakuwa shida yaani naweza kuvaa nguo mwaka huu na nikarudia mwaka ujayo.
My Style: Unaweza kuku-mbuka pochi zako za kubeba ziko ngapi?
Kajala: Nina pochi zaidi ya 30 na zote mara nyingi nanunua kua-nzia shilingi 70,000, 80,000 mpaka 100,000.
My Style: Vipi kuhusu mapenzi yana nafasi gani kwenye maisha yako?
Kajala: Nafasi yake kwangu ni ndogo sana maana sasa hivi niko mbio kuhu-siana na maisha yangu.
My Style: Unakumbuka Mara ya mwisho kwenda Kanisani lini?
Kajala: (Kicheko) Niliwahi kwenda mwaka jana lakini sasa hivi nitaanza kwenda kanisani tena maana ni jambo jema kumshukuru Mungu.
My Style: Haya nashu-kuru kwa ushiri-kiano wako.
Kajala: Asante sana karibu.
MAKALA: IMELDA MTEMA
0 Comments