Kama umekuwa ukifuatilia mzozo wa Ghuba bila shaka umesikia kuhusu mvutano uliopo kati Iran na Marekani.
Rais Donald Trump alikuwa amebakisha dakika 10 kuishambulia kijeshi taifa hilo na kwamba Marekani ilikuwa imesema itatuma wanajeshi 1000 Mashariki ya Kati kufuatia kile ilichotaja kuwa''uchokozi'' wa vikosi vya Iran.

Marekani iliilaumu Iran kwa kuzishambulia meli ya mbili za mafuta za Japan katika GhubaOman - jambo ambalo Irana imekanusha.
Pia kuna hali ya taharuki kwasababu Iran imesema itakiuka mkataba wa Kimataifa wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015.
Mvutano huu ulifikaja hapa?
A crude oil tanker Front Altair on fire in the Gulf of Oman,Haki miliki ya pichaEPA
Mfumo wa kuzalisha nguvu za umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia hutumiwa na mataifa mengi, Iraniliadhibiwa na kuwekewa vikwazo vya kufanya biashara na nataifa mengine baada ya kushukiwa huenda mpango wake wa nyuklia unatumiwa kuunda bomu kisiri.
Iran inasisitiza kuwa shughuli zake za kinyuklia ni salama- jamii ya kimataifa haijafanikiwa kuthibitisha kama hilo ni kweli au la.
Kati ya mwaka 2012 na 2016, Iran ilipoteza takriban pauni bilioni 118 baada ya kuwekewa vikwazo.
Mwaka 2015 Iran ilikubali kuweka saini mkataba wa kimataifa wa wa nyuklia ili Iruhusiwetena kufanya biashara na mataifa mengine duniani.
Lakini rais Donald Trump alijiondoa katika mkataba huo mwaka 2018 na kuiwekea tena vikwazo Iran.

Vikwazo hivyo ni vipi?

  • Ununuzi wa noti za Marekani unaofanywa na Iran.
  • Biashara ya dhahabu na vyuma vingine
  • Graphite, aluminium, chuma, mkaa na programu zinazotumiwa katika sekta ya viwanda
  • Ubadilishanaji wa fedha unaohusishwa na sarafu ya Iran
  • Vitendo vinavyohusishwa na ulipaji madeni ya Iran
  • Sekta ya magari ya Iran
Vikwazo hivyo viliathiri uchumi wa nchi hiyo- kwa sababu ililenga sekta yake kuu wa mafuta, na benki.
Iran ilijibu hatua hiyo kwa kukiuka baadhi ya vipengee katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia, na kuilaumu Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kulinda uchumi wa Iran dhidi ya vikwazo vya Marekani .
Lakini tatizo sio kuhusiana na mzozo wa nuklia pekee.
Siku wa Alhamisi Iran ilidungua ndege ya kijasusi ya Marekani isiyo na rubani kwa matai ya kuingia kwenye anga lake bila idhini- madai amabayo Marekani inapinga.
Rais Trump aliripotiwa kuidhinisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya Iran kwa kuidungua ndege yake lakini inadaiwa baadae alibadili msimamo huo.
Ni yapi yaliomo katika mkataba wa nuklia wa Iran?
Ni yapi yaliomo katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia?
Iran na mataifa mengine sita yalio na uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani kama vile- Marekani , Uingereza, Ufaransa, Urusi Ujerumani na China, yalikubaliana kuweka saini wa kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran mwaka 2015.
Mataifa hayo yalikuwa na hofu hkuwa Irana inaelekea kuunda silaha za nyuklia
Ili iweze tena kufanya biashara kimataifa, Iran ililazimika kusitisha mpango wake wa nyuklia.
Hatua aambayo ilihusisha kufunga baadhi ya viwanda vyake na kupunguza shughuli ya za uundaji wa silaha kwa kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kukagua mitambo yake ili kubainisha kama inafikia masharti yaliwekwa katika mkataba wa nyuklia.
Kwa niniDonald Trump alipinga mkataba huo?
Baadhi ya mammbo Rais Trump alisema kuhusu mkataba huo wa nyuklia
Rais Trump alisema mkataba huo unaegemea upande mmoja na kuongeza kuwa ni "mkataba mbaya sana" ambao Marekani ilikubaliana nao.
Alisema Iran inatumia hadi dola $100bn "kununua silaha kufadhili shughuli za kigaidi na kukandamiza watu" kwasababu ilikuwa imeondolewa vikwazo.
Badala yake, Bw.Trump alitaka mkataba huo ujadiliwe upya ili kudhibiti hatua ya jeshi la Iran kujiingiza katika mzozo wa Syria na Yemen.
Rais wa Marekani pia hakuridhishwa na wazo kuwa mkataba huo ulikuwa na tarehe ya ukomo - hatua ambayo kinadharia alihofia huenda ikaifanya Irana kurejelea tena mpango wake wa nyuklia baadae.
Mataifa mengine yalisemaje?
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na Rais wa Iran, Hassan RouhaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaziri mkuu wa Uingereza Theresa May alikutana na Rais wa Iran - Hassan Rouhani - mwaka 2016, kujadilia masuala ya Kimataifa
Mataifa ya Bara Ulaya yaliyohusika katika mkataba huo yamekuwa yakisema kuwa yanauunga mkono, lakini yanataka Iran kuutekeleza kikamilifu.
Mataifa ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani yallitishia kuiwekea tena vikwazo Iran.
Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alisema Uingereza"inatathmini njia zingine mbadala" ikiwa Iran itakiuka mkataba huo.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekuwa akiupinga mkataba huo na kupendekeza Iran iwekewe vikwazo mara moja ikikiuka mkataba huo.
Alionya kuwa: "Israel haitakubali Iran imiliki salaha za nyuklia."
Nini kitakachofuata?
Hormuz: Kwa nini eneo hili linaweza kuathiri maisha yako duniani
Iran imesema mataifa ya Ulaya yanaweza kuuokoa mkataba wa nyuklia kwa kuilinda dhidi ya vikwazo.
Pia kuna suala la kijeshi.
Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Hossein Salami anasema japo"Iran haitaki vita", kudunguliwa kwa ndege ya kijesusi ya Marekani isiokuwa na rubani ni ''ishara wazi kuwa wanataka vita''
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, Vikosi vya Marekani viko katika eneo hilo"kuzuia machafuko" na"na kulinda maslahi ya Marekani".
Pia huenda kuna suala la mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Saudi Arabia inaungamkonoMarekani na inailaumu Irankwa kushambulia meli za mafuta.
Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, ameoinya kuwa Iran na kuongeza kuwa Saudi Arabia "haitasita kukabiliana na tishio lolote".