Ni rasmi Jay-Z ndiye bilionea wa kwanza wa muziki wa hip hop ,limetangaza jarida la Forbes , baada ya kujijengea ufalme kutokana na muziki, mali, fasheni na uwekezaji.
Jarida hilo la Marekani limekadiria kuwa utajiri wa msanii huyo wa muziki wa rap sasa ni "jumla ya " dola bilioni $1.
Forbes linasema kuwa mumewe mwanamuziki Beyonce amefanikiwa kwasababu alijenga nembo zaidi tu ya kuziidhinisha.
Katika kuweka viwango vyake, Forbes ilipinga madai kuwa msanii huyo wa muziki wa kufoka na mzalishaji wake Dr Dre wamefikia kiwango cha ubilionea.
Jay-Z, alizaliwa hawn Carter, akakulia katika moja maeneo ya jiji la new York yenye sifa mbaya zaidi.
Alipata umaarufu mnamo mwaka 1996 kwa kazi yake iliyomuwezesha kutoa albamu ya Reasonable Doubt.
Albamu yake ya The Blueprint aliyoitoa mwaka 2001 iliongezwa mwezi Machi kwenye maktaba ya sajiri ya kitaifa ya Kongresi kwasababu ilionekana kama ya "kitamaduni, kihistoria au yenye umuhimu mkubwa".
Jarida la Forbes limesema lilikuwa limekadiria utajiri wa Jay-Z kwa kuongeza mali zake mbali mbali na "kutoa kiasi cha utajiri kinachomuwezesha kuishi maisha ya umaarufu ".
Miongoni mwa mali anazomiliki Jay-Z mwenyenye umri wa miaka 49 ni pamoja na:
Mkewe Beyonce anaripotiwa kuwa utajiri wa takriban dola milioni 335, alizotengeneza zaidi kutokana na muziki na kuidhinisha nembo, wawili hao wanamiliki zaidi ya dola bilioni 1 kwa miaka mingi.
Jay-Z, ambaye aliimba vibao kama "I'm not a businessman, I'm a business, man", ni mmoja wa watu wachache katika sekta ya burudani kufikia kiwango cha ubilionea ,kulingana na Forbes.
Mara nyingi kumekuwa na dhana kwamba Dr Dre alifikia kiwango cha ubilionea mwaka 2014 baada ya kuzalisha ngoma zake kwa kampuni ya Apple. Lakini mwaka jana Forbes ilitaja kiwango chake cha utajiri kuwa ni takriban dola milioni 770.
Kasseem "Swizz Beatz" Dean, wazalishaji wa ngoma kali zaidi za Jay-Z , waliliambia jarida la told Forbes kwamba mafanikio yake ni "makubwa zaidi ya hip-hop".
Alisema: " Ni utambulisho wa utamaduni wetu . Mtu anayeonekana kama sisi, anayesikika kama sisi, anayetupenda , aliweza kufikia kitu ambacho tulihisi kuwa kilikuwa juu yetu ."
Jay-Z anaonekana katika Kifuniko cha jarida la la hivi karibuni kabisa la Forbes kando na tajiri mwingine - tajiri zaidi -bilionea, Warren Buffet.
Inaelekea kuwa mwekezaji huyo wa muda mrefu aliyewekeza kwa miaka 40 , alibaini kitu maalum katika rapa huyo miaka michache iliyopita alipoliambia jarida la Forbes mwaka 2010: "Jay anafundisha darasa kubwa zaidi kuliko lile ambalo nitawahi kulifundisha. Kwa kijana mdogo anayekua,ni mtu wa kujijifunza kutoka kwake ."
|
0 Comments