Maafisa nchini Sudan kwa mara ya kwanza wamethibitisha kuwa hali siku ya juma wamekanusha madai kuwa watu 100 waliuawa na wanajeshi wakati wa maandamano na kukiri kuwa ni watu 46 waliyouawa katika purukushani hilo.
Madaktari wanaohusishwa na vuguvugu la waandamanaji wanasema idadi ya watu waliouawa na vikosi vya usalama wiki hii imepanda na kufikia zaidi ya watu 100.

Walisema miili 40 iliopolewa kutoka mto Nile mjini Khartoum siku ya Jumanne.
Awali mamlaka ilikuwa kimya kuhusiana na suala hilo lakini,maafisa wa wa wizara ya usalama mapema siku ya Alhamisi ilisema idadi ya waliyofariki ni 46.
Wanaharakati wa upinzani nchini Sudan wamekataa wito wa kufanya mazungumzo na baraza la kijeshi, ukihoji kuwa baraza haliwezi kuaminika baada ya msako wa nguvu dhidi ya waandamanaji.
Wakaazi wameiambia BBC kuwa wanaishi kwa uwoga katika jiji kuu la Khartoum.
Naibu mkuu wa Bwaraza hilo la Jeshi amepinga madai ya ukandamizaji na kuongeza kuwa wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya walikuwa wamejipenyeza katikati ya waandamanaji hao kufanya biahara zao.
"Hatutakubali vurugu kutokea na kamwe hatutarejea nyumakatika msimamo wetu. Hatuwezi kurudi nyuma. Lazima tuhakikishe nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria," alisema Mohammed Hamadan - ambaye pia anafahamika kama Hemedti - siku ya Jumatano.
Ripoti kadhaa kutoka mjini Khartoum zinaarifu kuwa kikosi maalum cha kijeshi kinachojulikana kama Rapid Support Forces (RSF), kimekuwa kikifanya msako katika barabra kadhaa za mji huo na kinawalenga raia.
Kikosi hicho zamani kilijulikana kama wanamgambo wa Janjaweed, na kinasadikiwa kuhusika na mauji na ukatili katika mzozo wa Darfur Magharibi mwa Sudan mwaka 2003.
Maafisa wa usalama walipelekwa katika makao makuu ya kijeshi kuwaondoa waandamanaji siku ya JumatatuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaafisa wa usalama walipelekwa katika makao makuu ya kijeshi kuwaondoa waandamanaji siku ya Jumatatu
Sudan imekua chini ya utawala wa kijeshi tangu Rais Omar al-Bashir alipopinduliwa mwezi Aprili.
Viongozi walioongoza vuguvugu la kutaka utawala wa kiraia kuongoza nchi hiyo, wamesema wamesitisha mawasiliano na serikali ya mpito ya kijeshi na kufanya mgomo.
Vikosi vya usalama vilifika maeneo ambayo watu walikua wakiandamana, mapema Jumatatu na sauti za risasi zilisikika kwenye picha za video.

Chanzo ni nini?

Waandamanaji wamekua wakikita kambi nje ya jengo la makao makuu ya jeshi tangu tarehe 6 mwezi Aprili, siku tano kabla ya kuangushwa kwa utawala wa Bashir.
Mwezi uliopita, waandaaji na majenerali watawala walikubaliana kuhusu muundo wa serikali mpya na muda wa mpito wa miaka mitatu kuelekea kwenye utawala wa kiraia.
Hawajaweza kuamua kuhusu ni upande upi hasa kati ya raia au jeshi kuchukua nafasi nyingi zaidi.
Idadi ya waandamanaji waliouawa Sudan yaongezeka
Mwezi uliopita, viongozi wa waandamanaji na majenerali wa jeshi walitangaza kuwa wamefikia muafaka wa muundo wa serikali ya mpito ya miaka mitatu ambayo itaandaa uchaguzi wa kiraia.
Lakini wamesema bado wanatakiwa kufanya maamuzi ya nani aingie kwenye baraza huru ambalo ndilo litakuwa na maamuzi ya mwisho kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitatu.
Hapajaweza kufikiwa makubaliano juu ya upande upi baina ya raia na wanajeshi uwe na wawikilishi wengi kwenye baraza hilo.
Deserted street in Khartoum, 4 JuneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarabara za mji wa Khartoum
Safari ya mabadiliko
19 Desemba 2018 - Maandamano yanalipuka baada bei ya mafuta na mkate kupanda
20 Desemba 2018 - Waandamanaji jijini Khartoum waanza kuimba nyimbo dhidi ya serikali wakitaka "uhuru, amani, haki"
22 Februari 2019 - Rais Omar al-Bashir atangaza hali ya hatari na kuvunja baraza la mawaziri
24 Februari - Maandamano yanaendelea licha ya vyombo vya ulinzi kutumia silaha za moto kutawanya waandamanaji
6 Aprili - Wanaharakati waanza kukita kambi mbele ya makao makuu ya jeshi wakiapa hawataondoka mpaka Bashir ang'oke madarakani
11 Aprili - Majenerali wa jeshi wanatangaza kuwa Bashir ameng'olewa uongozini laki waandamanaji wasalia wakitaka serikali ya kiraia
17 Aprili - Bw Bashir anapelekwa jela jijini Khartoum
20 Aprili - Mazungumzo baina ya viongozi wa kijeshi na wawakilishi wa waandamanaji yanaanza
13 Mei - Shabulio la risasi nje ya makao makuu ya jeshi linasabisha watu sita kuuawa
14 Mei - Majenerali na viongozi wa raia wanatangaza mapatano ya kuunda serikali ya mpito ya miaka mitatu
16 Mei - Mazungumzo yanaahirishwa baada ya jeshi kutaka baadhi ya vizuizi kuondolewa