Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akikata keki kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, keki aliyoandaliwa na watumishi wa ofisi yake kumpongeza wakati wa mkutano wa kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma kwa ofisi hiyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimlisha keki Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini cha ofisi hiyo Bw. Agustino Tendwa kwa niaba ya watumishi wa ofisi yake, wakati wa mkutano wa kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma Juni 22, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akihutubia watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea ambayo iliambatana na mafunzo kuhusu masuala ya utumishi wa umma kwa watumishi hao.Mkutano huo ulifanyika Juni 22, 2019 Ukumbi wa mikutano wa PSSSF Jijini DodomaKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na watumsihi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na watumsihi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma inayoendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Mazoea Mwera akifafanua jambo wakati mkutano huo. 
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU) 

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu Waaswa Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano kutoa huduma Bora kwa wananchi. 
Akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo leo (22 Juni, 2019) Jijini Dodoma , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza uwajibikaji, uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika utumishi wa umma ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali. 

“Kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi wa umma katika Ofisi yetu kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kuwa jambo hilo halikubaliki kamwe kwani vitendo hivyo vinazorotesha juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo “ Alisisitiza Mhe. Mhagama 

Akifafanua amesema kuwa mafunzo yaliyotolewa na Serikali kwa watumishi hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma yalijikita katika mada mbalimbali ikiwemo Rushwa mahala pa kazi , haki na wajibu wa watumishi wa umma. 

Aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inaweka mkazo katika kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vizuri pale wanapohitaji huduma hivyo ni wajibu wa kila mtumshi katika Ofisi hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wale wote wanaofika katika Ofisi hiyo na katika Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo. 

Kwa upande wake Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi amesema kuwa watumishi wa Ofisi hiyo watazingatia maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mhagama ili kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi. Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo wameadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kushiriki mafunzo ya kuwakumbusha taratibu na kanuni za utumishi wa umma, mafunzo kwa watumishi wanaotarajia kustaafu hivi karibuni. 

Ofisi ya Waziri Mkuu imeadhimisha wiki ya Utumishi ya Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali na kuhitimisha kwa mafunzo ya siku moja kwa watumishi wote yakilenga kuwakumbusha wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili hatimaye kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu inasema; “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji; kujenga utamaduni wa utawala bora., Matumizi ya tehama na ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi“