MAPEMA wiki hii Mbongo- Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alifunguka mengi kiasi cha kuibua vita mpya baina ya wanawake aliozaa nao, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mjasiriamali wa nchini Uganda na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto.
Vita hiyo imeibuka baina ya mashabiki wa Zari na wale wa Mobeto baada ya Diamond kusema kuwa Mobeto ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Dylan ni mwelewa kwani baada ya kuachana kilichobaki anatoa matumizi ya mtoto kama baba licha ya hapo awali kusumbuana kidogo.
Kwa upande wa Zari aliyezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan alisema hataki kuelewa kwamba wameachana kwani ‘ame-mblock’ kila sehemu ili asiweze kuwaona watoto wake wakati yeye ni baba mwelewa na anayewapenda watoto wake.
“Kwenye suala la watoto niko makini sana, ninahakikisha chochote nitakachoweza kumfanyia, nimfanyie, kuhusu watoto wangu ni kwamba mama yao (Zari) alini-block, ikabidi nikae kimya, naamini hasira zake zitaisha siku moja, wa hapa (Mobeto) alinielewa japo mwanzo tulisumbuana kidogo,” alisema Diamond.
Kutokana na maelezo hayo ya Diamond ilizuka vita ya maneno kwa pande hizo mbili yaani Timu Mobeto na Timu Zari ambapo walianza kupondeana huku wale wa Mobeto wakimtaka Zari akubali kuachika kama Mobeto alivyokubali na kukaa pembeni.
Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA
0 Comments