STAA anayefanya poa na wimbo wake wa Jini Kisirani, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amefunguka kuwa wanaume wote alioingia nao kwenye mapenzi walimtenda vibaya. Lulu ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa kila mwanaume aliyeingia naye kwenye mapenzi walimsaliti.


Amber Lulu alisema; “Kila mtu kaumizwa ila kwa sasa mapenzi hayana nafasi kama kazi yangu. Kazi yangu ina nafasi kubwa kuliko haya mapenzi, mtu kukusaliti ndiyo kunaumiza kuliko kitu chochote, kila mtu niliyekuwa naye kwenye mapenzi aliishia kunisaliti hivyo sitaki tena mambo hayo,” alisema Amber Lulu.

Amber lulu aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wasanii mbalimbali wakiwemo Young Dee, Barnaba Classic, Aslay, Rami Gallis na msanii kutoka nchini Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’.

Kwa sasa kuna tetesi kuwa anatoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Naftali Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.