Sebastien Desabre ameachia nafasi ya ukocha wa Uganda kwa ridhaa yake baada ya timu yake kuiaga michuano ya AFCON, shirikisho la soka nchini humo (Fufa) limetangaza Jumapili.
Uganda ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Senegal jijini Cairo siku ya Ijumaa katika mchezo wa hatua ya 16 bora.
Fufa imesema itamtangaza kocha mpya ''siku zijazo'' baada ya Desabre kuondoka huku akiwa amebakiwa na miezi mitano kumaliza mkataba wake.
''FUFA inatoa shukrani kwa mchango wa Desabre kwenye maendeleo ya soka la Uganda na timu ya Uganda Cranes'' Ilisema taarifa hiyo.
Desabre, 42 amekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uganda tangu aliposaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo mwezi Desemba mwaka 2017.
Kabla ya Cranes kupoteza mbele ya Senegal siku ya Ijumaa. wachezaji waligomea mazoezi mzozo uliokuwa kati ya wachezaji na Fufa kuhusu malipo.
|
0 Comments