Hatua ya Mahakama kuu ya nchini Afrika Kusini kuzuilia kuruka ndege ya Air Tanzania imeendelea kuzua mjadala kuhusu chanzo chake.
Mpaka sasa Mamlaka nchini Afrika Kusini haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam.
Lakini Kwa mujibu wa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ndege hiyo imezuiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya mjini Johannesburg.
Ripoti ya baadhi za vyombo vya habari nchini Tanzania zinaashiria kuwa abiria waliokuwa ndani ya ndege ya Air Tanzania iliyozuiliwa kuondoka katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo mjini Johannesburg wametafutiwa usafiri mbadala.
Gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi amesema ''Kuna safari nyingi zitakazoathiriwa ktokana na kushikiliwa kwa ndege hiyo aina ya Air Bus A220-300''
Bwa. Matinde ameliambia Mwananchi kuwa abiria waliokata tiketi wataarifiwa iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote ama ipo kama ilivyopangwa.
Tayari Shirika hilo limetoa taarifa rasmi kupitia mtandao wake wa Twitter kuwaomba radhi wateja wake na kuongeza kwamba kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake itafanyia marekebisho safari zake
Ruka ujumbe wa Twitter wa @AirTanzania
94 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @AirTanzania
Msemaji wa mkuu wa serikali ya Tanzania ameiambia BBC kuwa wanasheria wa wa nchi hiyo wamewasili nchini Afrika Kusini kufuatilia suala hilo na kwamba wakikamilisha mchakato huo watatoa taarifa kamili.
Taarifa iliyotolewa Ijumaa usiku na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Leonard Chamuriho ilieleza kuwa serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu inafuatilia suala hilo.
Baadhi ya raia wa Tanzania wamekuwa wakijadili nini huende imeeifanya mahakama ya nchini Afrika Kusini kuzuilia ndege hiyo
@majanimabichi ameandika katika Twitter yake akiuliza: Kwa nini mahakama ikamate/izuie ndege? Kuna jambo limejificha nyuma ya pazia. Toeni sababu.
@PaternusP aliandika:Tulitazame kwa umakini na kidiplomasia. Kutikiswa lazima watatutikisa kutupima REACTIONS zetu. Hakuna haja ya kupaniki juu ya jambo hili. Adapt, Improvise, Overcome.
@catfish88854732 aliandika South Africa ; mahakama ziko huru .Rais wa Sauzi kamwe hawezi kuingilia mahakama.
Wengine walichukua jukumu la kuwafafanulia wenzao maana ya hatua hiyo
Ruka ujumbe wa Twitter wa @Mtwale_
See MOHAMMED MAULID MTWALE (M³)'s other Tweets
|
0 Comments