JAJI Mkuu wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba (BSS) Rita paulsen a.k.a Madam Rita amesema bado shindano hilo ni ganda la ndizi kwa vijana wenye nia ya kufikia mbali kwenye sekta muziki.

Madam Rita ameeleza kitu kikubwa hasa kinachomsukuma kila mwaka kuendelea kujitolea kusaidia vijana ni kutokana na wengi wao kuonyesha nia, jitihada na malengo yao kufika mbali na kuwa wasanii wazuri kama wengine au hata kuzidi uwezo wao.

"Wapo wasanii ambao tunajivunia uwepo wapo na tunajitoa kifua mbele kuona ni zao letu la (Bss ) Kama Kala Jeremiah, Mina Atick, Leah Moudy, Jumanne Iddi, Haji, Pascal Cassian ,Walter Chilambo, Kayumba, Frida Amani, Peter msechu ambao wengi tuliwatoa mikoani na kuwafungulia njia ya kuonyesha vipaji vyao kwa watanzania,"


Licha ya kuwepo kwa mafanikio mengi ambayo amepata lakini bado anakumbana na kasumba ya baadhi ya watu kuchukulia shindano hilo kama nguvu ya soda kwa washindi kutosikika kwa kipindi fulani au hata kutoonekana Tena kwenye taswira ya muziki pamoja na kukatishwa tamaa na kupigwa vita kwa baadhi ya watu.

" Shindano hili lipo kwa ajili ya kukusaidia kutafuta mashabiki wa awali ambapo Kama msanii mwenyewe hatoonyesha ujuzi zaidi ya kile wanachokiona mashabiki inakua ni kazi bure kwani naamini ukishikwa mkono na wewe inabidi umpe moyo yule aliekushika.

"Kuna baadhi wapo na wanaendelea na muziki vizuri kutokana na jitihada zao za kupigania kile ambacho wanakiu nacho na wengine hawaendelei pengine kwa sababu tofauti tofauti mtu wa kusimamia kazi zake anakua sio mzoefu,starehe kupita kiasi ameshakua maarufu anajisahau nini anatakiwa kufanya wakati huo"


Pia Madam Rita amesema kwa sasa msimu wa 10 wa Bss umerudi tena kwa kishindo huku majaji wapya wakiwa ni wakongwe kwenye Muziki wa Bongofleva.

"Dullysykse, Lady Jjay Dee  watakuwa nasi pamoja Kama majaji wapya katika msimu huu wa 10 wa shindano hili tutegemee vipaji vingi na vizuri,"

Aidha Rita amefafanua mikoa watakayofika kufanya usahili ni Arusha Septemba 28 hadi 29, Mwanza Oktoba 4 hadi 5 , Mbeya Oktoba 10, Dodoma Oktoba 17 na huku Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni 23, 24 na 25 Oktoba mwaka huu.

"Na vipindi vitaonekana katika King'amuzi cha startimes kupitia  chaneli ya ST Swahili.

    
   Na.Khadija Seif, Michuzi TV