La Liga imeitaka mechi kali ya El Clasico mnamo tarehe 26 Oktoba kuhamishwa kutoka uwanja wa Barcelona wa Nou Camp hadi katika uwanja wa Real Madrid kufuatia hofu ya kutokea kwa maandamano.
Kumekuwepo na maandamano mjini Barcelona baada ya wanaharakati tisa wanaopigania kujitenga kwa Catalan kufungwa jela siku ya Jumatatu.
La Liga iliwasilisha ombi hilo kwa serikali ya Uhispania na klabu zote mbili zitaulizwa maono yao.
Awali BBC Sports inaelewa kwamba Barcelona ingetaa ombi hilo kwa kuwa klabu hiyo inaona ombi hilo la kuhamishwa halihitajiki.
Unaweza pia kusoma:
Maandamano zaidi yanatarajiwa katika mji huo katika siku ya mechi hiyo na shirika la marefa linasema kwamba hatua hiyo inajiri katika mazingira yasioweza kuepukika.
Kamati ya ushindani katika shirikisho hilo inatarajiwa kufanya uamuzi wake katika siku chache zijazo.
Barcelona na Real Madrid hazikuhusishwa katika ombi hilo la La Liga na kwamba hakujakuwa na tamko lolote rasmi kutoka kwa klabu zote mbili.
Inamaanisha kwamba mechi hiyo iliyotarajiwa kuchezwa mwezi Machi sasa itafanyika mjini Barcelona.
Unaweza pia kusoma:
Shirikisho la soka katika jimbo la Catalan lilisimamisha mechi zote katika eneo hilo siku ya Jumatatu, ijapokuwa uamuzi huo hautaathiri kivyovyote mechi za La Liga ama timu ya taifa ya Uhispania.
Catalonia ni jimbo huru kaskazini mashariki mwa Uhispania na kura ya maoni ya tarehe mosi Oktoba 2017, ambayo ilitangazwa kuwa haramu na mahakama ya kikatiba ya Uhispania , ilisema kwamba asilimia 90 waliunga mkono uhuru wao, hatahivyo walioshiriki katika kura hiyo ni asilimia 41 pekee.
Wanaharakati hao wa kupigania kujitawala kwa jimbo hilo walipatikana na hatia ya kuasi kufuatia jukumu lao katika kura hiyo ya maono na kupewa kifungo cha miaka tisa na 13 na mahakama ya kilele ya Uhispania.
Kufuatia hukumu hiyo, Barcelona ilisema: Jela sio suluhu.
Mabingwa hao wa Uhispania waliongezea: Sasa zaidi ya ilivyokuwa klabu hiyo imetaka viongozi wote wa kisiasa kuongoza mchakato wa majadiliano ili kutatua mzozo huo, ambao unahitaji kuruhusu kuwachiliwa kwa viongozi hao.
Klabu ya Barcelona pia imeunga mkono familia zote za viongozi ambao wamenyimwa uhuru wao.
|
0 Comments