Mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Tanzania anayekabiliwa na mashtaka matatu ya kuhujumu uchumi wa nchi bado hajakiri mashtaka baada ya kesi yake kuahirishwa hadi Oktoba 6.

Hatua ya Kabendera kuomba msamaha imekuja baada ya Mkurugenzi mkuu wa mashtaka wa serikali kuwasilisha majina ya watu 467 ambao tayari waliomba msamaha kwa makosa ya kuhujumu uchumi, jambo ambalo linawaruhusu washukiwa hao wanaosubiri kesi zao kuweza kuomba waachiliwe.
Hata hivyo wakili wa Bwana Kabendera, Jebra Kambole amesema kuwa mteja wake hakuwasilisha ombi la msamaha kwasababu haweza kufanya hivyo.
Wakili wa mwandishi huyo wa habari Jumanne alimuomba rai John Pombe Magufuli amsamehe mteja wake , ambaye anasema hana hatia.
Kabendera akishauriana na wakili wake Jebra Kambole katika mahakama ya Kisutu
Image captionKabendera akishauriana na wakili wake Jebra Kambole katika mahakama ya Kisutu
Kabendera alishtakiwa mwezi Agiosti kwa kosa la kupanga uhalifu, kushindwa kulipa kodi na wizi wa pesa.
''Kufanya kazi kama mwandishi wa habari ni changamoto na kama Kabendera kwa kiasi fulani alikosea , tunaomba msamaha. Kama rais anasikia hili , kwa unyenyekevu tunuomba kulingalia hili na kama mawakili tuko tayari kufanya kitu kinachohitajika kumuwezesha kuwa huru,'' Wakili Jebra Kambole aliwaambia waandishi wa habari.
Waendesha mashtaka wameiambia mahakama kuwa uchunguzi wao bado haujakamilika na kesi hiyo ikaahirishwa hadi tarehe 11 Oktoba 11.
Kabendera bado anapokea huduma za matibabu gerezani kwasababu imekuwa ni vigumu kwake kutembea kutokana na kupooza kwa mguu wake wa kulia, na ana matatizo ya kupumua, alisema Kambole.