KLABU ya Yanga imemtangaza kocha wao mpya ambaye ni raia wa Ubelgiji aitwaye Luc Eymael (60) ambaye anatarajia kutua rasmi Zanzibar saa 8:30 mchana leo Alhamisi, Januari 9, 2020.

Eymael anatua kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Mkongomani, Mwinyi Zahera, ambaye mwishoni mwa mwaka jana alitimuliwa na timu hiyo kisha kumkabidhi kocha wa muda, Charles Mkwasa, anayeendelea kuinoa timu hiyo sasa.

Kocha Luc Eymael hapo awali alikuwa golikipa. Alicheza takribani michezo 729 kwa miaka 25 kuanzia mwanza 1975-2000.
Amehudumu kama kocha kwa miaka 20 (1999-2000). Ana leseni ya Uefa Pro aliyopata 2007.

VILABU ALIVYOFUNDISHA  kwa miaka 20;
1999–2003 RUS Sartoise
2003–2004 Weywertz
2004–2007 Jeunesse Lorraine Arlonaise
2007–2009 RFC Spy
2009–2010 Royal Racing Club Hamoir
2010–2011 AS Vita
2011–2012 Missile
2012 MC Oran
2013 A.F.C. Leopards
2014 Rayon Sports
2014–2015 JS Kairouan
2015 Al-Nasr
2015–2016 Al-Merrikh
2016–2017 Polokwane City
2017–2018 Free State Stars
2018–2019 Tala’ea El Gaish
2019– Black Leopards

Mataji akiwa kama kocha;
Akiwa na AS Vita
Linafoot (1):
Winners 2010
Super Coupe du Congo (1):
Winners 2011
Akiwa na Missile
Gabon Championnat National D1 (1):
Winners 2010–11
Akiwa na A.F.C. Leopards
Kenyan Premier League (0):
Runners-up 2013
FKF President’s Cup (1):
Winners 2013
Akiwa na Rayon Sports
Rwanda National Football League (0):
Runners-up 2013–14
Akiwa na Free State Stars
Nedbank Cup (1)
Winners 2018.