MSANII wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amesema kuwa jina ambalo analolitumia hivi sasa la Gift ni kwamba alijipachika ili tu aendane na wakati na pia hakulipenda jina la Zawadi.
Akizungumza na CHANZO CHA HABARI, Gigy alisema kuwa alipokuwa msichana mdogo akiwa ameanza kujua mambo ya mjini, aliona kuitwa jina la Zawadi, ni kama litamzibia vitu, hivyo kwa vile jina lake linaweza kugeuzwa, akaamua kujiita Gift.
“Kiukweli jina la Zawadi lilikuwa linanikera sana lakini kwa vile nilishaanza kujua mambo mengi ya mjini, kwangu haikuwa kazi kulibadilisha kutoka kwenye Kiswahili kwenda kwenye Kiingereza na bahati nzuri likakubalika vizuri mpaka leo,” alisema Gigy ambaye kila kukicha haishi vituko kwenye mitandao ya kijamii.
0 Comments