Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi binafsi wa maiti, hatua ya Chauvin ilichangia kifo cha wiki iliyopita cha Mmarekani mweusi George Floyd, ambacho kilisababisha maandamano makubwa nchini Marekani.
Katika video hiyo iliozua ghadhabu, Chauvin- afisa mzungu wa polisi, anaonekana akimzuilia chini Floyd akitumia goti lake kwenye shingo, huku Floyd akilalamika kuwa hawezi kupumua.

Lakini Chauvin, ambaye tayari amefutwa kazi kwa kutekeleza mauaji bila kukusudia, hakuwa peke yake.
Alikuwa ameandamana na maafisa wenzake Thomas Lane, JA Kueng na Tou Thoa , ambao walishuhudia kukamatwa kwa Floyd bila kuingilia kati hali iliyosababisha kifo chake .
Maafisa wote wanne wanahudumia kitengo cha polisi cha Minneapolis (MPD).
Baada ya video ya tukio hilo baada ya kanda ya video kutolewa, Mkuu wa MPD, Medaria Arredondo, aliwafuta kazi.
Ijumaa wiki iliyopita, Chauvin alikamatwa na kushitakiwa kwa mauaji bila ya kukusudia.
Lakini maafisa watatu waliosalia walifanywa nini?

Sababu ya maandamano

George Floyd, alikuwa baba ya msichana wa miaka sitaHaki miliki ya pichaTWITTER/RUTH RICHARDSON
Image captionGeorge Floyd, alikuwa baba ya msichana wa miaka sita
"Kwanini maafisa watatu kati ya wanne bado hawajachukuliwa hatua wakati familia ya George Floyd inakabiliwa na majonzi?" Aliuliza Alicia Garza, mmoja wa waanzilishi wa vugu vugu la Black Lives Matter .
Hilo ndilo swali ambalo pia Philonise, ndugu wa marehemu George Floyd, anajiuliza.
"Nataka kujua ikiwa ndugu yangu atatendewa haki na ikiwa maafisa wote waliohusika na kifo chake watakamatwa na kufungwa," Philonise alikiambia kituo cha televisheni cha CNN siku ya Jumapili, akielekeza swali hilo kwa mkuu wa kitengo cha polisi cha Minneapolis.
Hakuna hata mmoja kati ya maafisa hao watatu aliyeshitakiwa kwa kosa lolote, licha ya shinikizo kutoka kwa familia ya Floyd na waandamanaji, ambao baadhi yao wameapa kuendelea na maandamano hayo hadi pale maafisa hao watakapokamatwa.

Walihusika vipi na tukio hilo?

Maafisa wote watatu walionekana katika video inayoonesha kukamatwa kwa Floyd. Stakabdhi za kisheria zinajumuisha jukumu la kila mmoja wa katika tukio hilo ambalo lilisababisha kifo.
Kifo cha Floyd: Wamarekani weusi wasema 'hawako salama'
Baada ya mwenye duka kuwasilisha malalamishi kwamba kuna mtu aliyejaribu kumlipa kwa kutumia dola 20, maafisa wa kwanza kufika dukani hapo walikuwa Lane na Kueng.
Msimamizi wa duka hilo aliwafahamisha kuwa mshukiwa - Floyd - alikuwa ndani ya gari lililoegeshwa hatua chache kutoka duka hilo.
Walipomfikia walimpata akiwa na watu wengine wawili ndani ya gari.
Polisi wote walikuwa wamevalia kamera inayorekodi mienendo yao wakiwa kazini. Kanda hiyo kufikia sasa haijatolewa kwa umma lakini zimewasilishwa kwa wachunguzi wa kesi hiyo.
George FLoyd anakumbwa na wakaazi wa MinneapolisHaki miliki ya pichaAFP
Image captionGeorge FLoyd anakumbwa na wakaazi wa Minneapolis
Kwa mujibu wa stakabadhi za kisheria, Lane alizungumza na Floyd, ambaye alikuwa amekaa katika kiti cha dereva, huku Kueng akizungumza na mtu aliyekuwa amekalia kiti cha upande wa abiria.
Dakika chache baadae, Lane alitoa bastola yake na kumuelekezea Floyd, akimtaka anyanyue juu mikono yake. Floyd aliitikia agizo hilo na Lane akarejesha bastola yake.
Lane baadae alimtaka atoke ndani ya gari huku akionesha ishara ya kutaka kumfunga pingu, ni hapo ambapo Floyd alijaribu kupinga hatua hiyo, kwa mujibu wa mashitaka rasmi.
Tou ThaoHaki miliki ya pichaDARNELLA FREZIER/FACEBOOK
Image captionTou Thao ni mmoja w maafisa waliohusika katika kukamtwa kwa Floyd
Baada ya kufungwa pingu, video inamuonesha Floyd akichuchumaa, kutii amri ya Kueng.
Maafisa wengine wawili, Chauvin na Thao, waliwasili muda mfupi baadae.
Derek ChauvinHaki miliki ya pichaDARNELLA FRAZIER
Image captionDerek Chauvin ni mmoja wa maafisa wanne waliofutwa kazi baada ya kukamatwa kwa Floyd
Baada ya kufungwa pingu, bwana Floyd alikubali kushikwa huku bwana Lane akielezea alikuwa anakamatwa kwa kutoa pesa bandia.
Ni wakati maafisa wa polisi walipojaribu kumuingiza bwana Floyd katika gari lao ndiposa mvutano ukatokea.
Baada ya mvutano kidogo wa kujaribu kumuingiza Floyd ndani ya moja ya magari ya polisi, Chauvin alimzuilia chini uso huku uso wa mwanamume huyo ukiwa umebamizwa sakafuni, nae Lane akishikilia miguu yake na Kueng akizuilia chini sehemu ya mgongo.
Thao alikuwa amesimama kando ya gari hilo.
Línea

Tunachokifahamu kuwahusu maafisa hao

  • Hakuna maelezo ya kina kuwahusu maafisa hawa.
  • Tou Thao aliwahi kushitakiwa mwaka 2017 kwa madai ya utumizi wa nguvu kupita kiasi.
  • Kesi hiyo ilikamilishwa baada ya kuamuliwa. Malalamishi mengine sita yaliripotiwa dhidi ya Thao. Tano kati ya kesi hizo zinaendelea. Rekodi zilizotolewa kwa umma hazina maelezo zaidi kuhusiana na kesi hizo.
  • Thomas Lane alijiunga na MDP mwaka 2019. Hakuna rekodi yoyote ya mashitaka dhidi yake.
  • Hakuna taarifa kuhusu historia ya kikazi ya J. Alexander Kueng. Pia hakuna rekodi yoyote ya mashitaka dhidi yake.