Goli la Grealish lilikua ni la 10 katika msimu uliovutia
Ligi kuu ya England imemalizika jioni ya leo baada ya michezo ya raundi ya thelathini na nane kuchezwa huku Liverpool wakiwa ndio mabingwa wa ligi hiyo kwa jumla ya alama 99.
Timu ambazo zingeshuka daraja na ambazo zinakwenda kucheza michuano ya ulaya msimu ujao ndio kitu kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu na wapenda soka wengi duniani
Katika Ukanda wa Afrika mashariki macho na masikio yalikuwa katika mchezo wa mwisho wa Aston Villa, klabu anayocheza Mtanzania Mbwana Samata, kama itashuka ama itasalia kwenye ligi kuu , hata hivyo Aston Villa imesalia kwenye ligi kuu baada ya kwenda sare ya goli 1-1 na West Ham United.
Kusalia kwa Villa kwenye ligi kuu ya England, kufanya mchezaji kutoka ukanda wa Africa Mashariki Mbwana Samata kuendelea kuuwakilisha ukanda huu.
Baada ya Liverpool na Man City kujihakishia kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao mapema, leo hii Man United na Chelsea nao wamejikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa ya ulaya.
Man United wakiwa ugenini katika dimba la King Power wamewafunga wenyeji wao Leicester City kwa magoli 2-0 kwa magoli ya Bruno Fernandes kwa mkwaju wa penati na Jesse Lingard na hivyo kumaliza ligi katika nafasi ya tatu.
Leicester Licha ya kupoteza mchezo huu kwa kufungwa nyumbani wao wamepata anfasi ya kucheza michuano ya usiku mdogo wa ulaya Europa ligi kwa kumaliza katika nafasi ya tano wakiwa na alama 62.
Chelsea wao wamemaliza ligi wakiwa na nafasi ya nne na tiketi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao baada ya kuwachapa Wolverhampton Wanderers kwa 2-0 kwa magoli ya Mason Mount na Olivier Giroud.
Tottenham Hotspur wakiwa ugenini katika dimba la Selhurst Park wamevutwa shati na wenyeji Crystal Palace kwa kufungana goli 1 - 1, hata Hivyo Tottenham wanafuzu kushiriki michuano ijayo ya Europa ligi.
Timu zilizoshuka daraja ni Norwich City, ambao wamefungwa goli 5-0 na Man City, Watford nao wameteremka daraja kwa kuchapwa na Arsenal kwa goli 3-2.
Licha ya ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Everton klabu ya AFC Bournemouth nayo imeshuka daraja kwa kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya 17 kwa jumla ya alama 34 wakizidiwa alama moja tu Aston Villa.
Matokeo ya michezo yote ya leo ya Epl
Arsenal 3 - 2Watford
Burnley 1 - 2 Brighton & Hove Albion
Chelsea2 - 0Wolverhampton Wanderers
Crystal Palace 1 - 1 Tottenham Hotspur
Everton 1 - 3 AFC Bournemouth
Leicester City 0 - 2 Manchester United
Manchester City 5 - 0 Norwich City
Newcastle United1 - 3 Liverpool
Southampton 3 - 1 Sheffield United
West Ham United 1 - 1 Aston Villa