Maafisa wa afya katika eneo la tukio walijaribu kumsaidia mtu aliyekuwa amepigwa risasi kifuani
Maelezo ya picha,

Maafisa wa afya katika eneo la tukio walijaribu kumsaidia mtu aliyekuwa amepigwa risasi kifuani

Picha kutoka eneo la tukio ziliwaonesha maafisa wa afya wakimuokoa kile kilichoonekana mzungu mmoja.

Maafisa wa polisi hawajatoa utambuzi ama kufichua iwapo ufyatuaji huo wa risasi ulihusishwa moja kwa moja na ghasia zilizotokea katika eneo hilo.

Barabara za Portland zimekuwa zikishuhudia mandamano ya mara kwa mara dhidi ya unyayasaji unaotekelezwa na maafisa wa polisi katika majuma ya hivi karibuni.

Mji huo umeshuhudia maandamano dhidi ya unyanyasaji unaotekelezwa na polisi pamoja na ubaguzi wa rangi tangu polisi walipomuua mtu mweusi George Floyd katika mji wa Minneapolisi tarehe 5 mwezi Mei na kusababisha hisia kali nchini humo na hata kimataifa.

Maafisa wa polisi wa kijimbo walitumwa na rais Trump kaika eneo la Portland mwezi Julai katika kile kilichoonekana hatua ya kuzuia ghasia.

Maafisa wa afya walithibitisha kwamba mwathiriwa alikuwa tayari ameaga dunia.

Mtu huyo alikuwa amevalia kofia iliohusishwa na kundi la mrengo wa kulia la Patriot Prayer kulingana na gazeti la New York Times.

Picha nyengine zinawaonesha maafisa wa polisi wakijaribu kumzuia mtu ambaye alikuwa na marehemu.

Maafisa wa polisi wakimzuia mtu mmoja wakati wa ghasia za Portland
Maelezo ya picha,

Maafisa wa polisi wakimzuia mtu mmoja wakati wa ghasia za Portland

Kinachojulikana kuhusu ufyatuzi huo wa risasi

Mkutano huu wa rais Trump ni watutu kwa mfululizo.

Katika taarifa siku ya Jumamosi jioni, maafisa wa polisi mjini Portland walisema: Maafia wa polisi walisikia sauti za milio ya risasi kutoka eneo la barabara ya Kusini mashariki katika barabara ilio kusini mashariki ya Alder.

Walijibu na kumpata mmoja ya waathiriwa akiwa na jeraha la risasi katika kifua chake.

Ni nini kilichosababisha ufyatuaji huo wa risasi?

Tukio hilo linajiri baada ya vita kuzuka kati ya wafuasi wa Trump na waandamanaji wa Black Lives Matter katikati ya mji.

Hofu ilizuka baada ya msafara wa magari 600 yaliokuwa yakipeperusha bendera na kuwabeba wafuasi 1000 wa Trump kukutana katika duka moja kubwa katika kaunti ya Clackmas kandokando ya mji huo kabla ya kuingia mjini Portland.

Kanda ya video iliwaonesha baadhi ya watu wakirusha maji yanayowasha macho kwa waandamanaji wa BLM waliojaribu kuwazuia kuingia mji huo kwa kufunga barabara.

Maafisa wa polisi waliripoti visa vya ghasia kati ya waandamanaji hao wa pande pinzani na kusema kwamba baadhi yao wamekamatwa.

Siku hiyo ilianza kwa msafara wa magari wa wafuasi wa rais Trump uliokingia mjini Portland
Maelezo ya picha,

Siku hiyo ilianza kwa msafara wa magari wa wafuasi wa rais Trump uliokingia mjini Portland

Ghasia hizo zinajiri kufuatia hatua ya chama cha Republic kumpatia tiketi ya kuwania urais rais Donald Trump .

Akikubali uteuzi wake katika hotuba aliotoa katika ikulu ya Whitehouse , aliutaja mji wa Portland kama mji mwengine unaongozwa na viongozi wa Democrat uliojaa ghasia, maandamano, wizi na uchomaji moto wa mali.

Ghasia hizo zinajiri baada ya shambulio la mtu mweusi Jacob Blake mjini Winsconsin.

Jacob Blake alijeruhiwa vibaya wiki iliopita baada ya kupigwa risasi mgongoni mara saba na afisa wa polisi wa Kenosha alipokuwa akiingia katika gari lake.

Rais Trump alisema kwamba atatembelea eneo la Kenosha ambalo limezongwa na ghasia.