Baadhi ya picha alizozitumia Grace kuwatafuta ndugu zake kwenye mitandao ya kijamii akiwa na matumaini ya kuwapata

Baada ya vita na mauaji ya kimbari nchini Rwanda Grace Umutoni amekua akiishi kwa majonzi makubwa kwa muda wa miaka ishiri yote baada ya mauaji hayo kwa kutomjua mtu yeyote ambaye ana uhusiano nae wa damu.

Ilikua ni Jumatano ya wiki hii tu ambapo maisha yake yalibadilika kabisa "niliona muujiza ", na sasa nina mabinamu, mashangazi na haya wajomba, ambao wanasema, wanafuraha isiyo na kifani.

Kwa sasa ana umri wa miaka 28 na anafanya kazi ya uuguzi yani nesi. Wakati mauaji ya kimbari yalipotokea Rwanda alikua na umri wa miaka 2 tu na alibahatika kubusurika na mauaji hayo katyika wilaya ya Ngoma ambako alilelewa na mwanamke mzee mwenye umri wa miaka 85.

Katika mahojiano na BBC , Grace Umutoni anasema alipopata akili na kujitambua alikuta amepewa jina rafiki, na alikua wakati huo akiishi katika kituo cha yatima katika eneo la Ndera lililopo katka mji mkuu wa Rwanda Kigali, ambako baadae aligundua kuwa kuna ndugu yake anayefahamika kwa jina Yves, kaka yake mdogo ambaye waliletwa pamoja katika kituo hicho cha yatima mwaka 1994.

Anasema kuwa baadae aliambiwa kuwa nyumbani kwao palikua panaitwa Nyamirambo, lakini hakuwafahamu wazazi wake, jinsi walivyouliwa, na hata hakuwa na taarifa zozote ni jinsi gani binafsi aliweza kunusurika na mauaji ya kimbari ... hakujua ni majina gani alikua amepewa na wazazi wake kabla hawajauawa.

Mamia ya watu ambao wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambao wakati huo walikua ni watoto, kwa sasa ni watu wazima nab ado wanawatafuta watu wa familia zao, kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC), unaozikutanisha familia zenye zilizopoteana na wapendwa wao wakati huo.

Nini kilichomtokea 'Rafiki'?

Nyumbani kwetu tulikua watoto watatu , Yves , mini, halafu na mtoto mwingine mchanga , sikumbuki jina lake na sikumbuki kama alikua ni wa kiume au wa kike - anasema Umutoni

Yves alikua amepata majeraha, kwasababu walimpiga risasi ubavuni , ndivyo nilivyoambiwa na watu na tulipofika kwenye kituo cha yatima Ndera alikufa.

Niliambiwa taarifa hizo baada ya kuwa mtu mzima'', aliiambia BBC.

Alibatizwa katika kituo cha yatima na huko ndiko alikopewa majina Grace Mutoni

Rafiki
Maelezo ya picha,

'Rafiki' ndio jina pekee ambalo alifikiria lingeweza kutambulisha... huu ni ujumbe aliouambatanisha na picha zake wa kuwatafuta watu wa familia yake mwezi wanne mwaka huu

Kabla Umuto aanze shule ya msingi mwanamke msamaria mwema aliyemuokota alifariki dunia kwa ugonjwa na hapo ndipo alipoendelea kulelewa na mama yake mwanamke huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 85.

Anasema katika maisha yake alikua akiwaza ni jinsi gani angeliweza kuwapata ndugu wa familia yake kando na walimlea.

"Lakini kusema kweli familia iliyonitunza ulinitunza kwa upendo kwasababu hata kusoma ni wao walionifundisha. Mwanamke huyo mzee ndiye aliyenitunza na hakuwa na kazi , lakini alinisaidia kila awezavyo maisha yakaendelea ".

Umutoni avuga ko yahoranaga agahinda ariko akagira n'ikizere ko azabona abo mu muryango we
Maelezo ya picha,

Grace Umutoni anasema kuwa maisha yake yalikua ni ya majonzi , lakini alikua na matumaini kuwa siku moja atawaona ndugu zake wa damu

Alipomaliza kusoma Chuo Kikuu, msichana mmoja rafiki yake alimshauri awatafute ndugu zake kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Anasema: " Mwanzoni nilikua nikitaka kuweka matangazo kwenye mitandao ya kijamii kuwatafuta jamaa zangu , watu walikua wananikatisha tamaa wakiniambia utaanzia wapi ? Haujui majina ya wazazi wako isipokua jina Yves tu na kwamba mlikua mkiishi Nyamirambo na wengine wananiambia labda hata hamkua mkiishi huko, unajisumbua ...nilikua nakata tamaa".

Muujiza

Tarehe 07/04/2020, akisaidiwa na rafiki yake walitengeneza picha yake wakaandika maneno ya kutafuta familia wakaiweka kwenye mitandao ya kijamii ya kijamii.

Umutoni anasema i: "Tulitengeneza tupicha twangu nikiwa mdogo na twingine nikiwa mtu mzima tukatuambanisha na tangazo la kuwatafuta ndugu zangu kwenye mitandao ya WhatsApp, Instagram, na Twitter.

Baadae nikaona watu wanaojibu kwenye picha hiyo wakisema etu huyu ni mtoto wetu '.

Baadae alikuja mwanaume mmoja ambaye aliniambia kwamba yeye ni mjomba wangu , akamwambia kuwa taarifa alizoziona kwenye mitandao ya kijamii zilimfanya ahisi kuwa Umutoni alikua ni mtoto wa dada yake.

Umutoni anasema kuwa mwanaume huyo alimwambia kuwa anafanana sana na marehemu mama yake. Lakini anasema kuwa pia alipomuona mwanaume huyo aliona kweli anafanana nawe kidogo.

We na nyirarume babafashe ikizamini cya DNA basanga bahuje kuri 82%
Maelezo ya picha,

Grace Umotoni alipata ana uhusiano wa damu na mjomba wake kwa 82% baada ya kuchukua kipimo cha vinasaba

"Tuliongea, na baadae tukakubaliana kuchukua vipimo vya vinasaba(DNA) ili kuthibitisha ukweli kwamba tuna undugu wa damu ."

''Tarehe 16 mwezi wa saba ndipo tulipofanya kipimo cha DNA na majibu yalipotoka kweli tukakuta tuna undugu wa damu'', anasema Umutoni na kuongeza kuwa:

"Walipata tuna uhusiano wa 82%, ya undugu, walitupatia matokeo tukiwa pamoja , siwezi kusimulia nilivyojihisi kumpata mtu mwenye uhusiano na mimi, hadi sasa sijaamini, huwa wakati mwingine nafikiri ninaota.

"Unajua miaka yote hii iliyopita nikifikiri kuwa sina mtu yeyote mwenye undugu wa damu... Nimekua nikifikiri nipo hapa dunaini peke yangu... Nilishituka sana kwa hiyo kumuona mtu mwenye uhuziano na mimi wa damu na kupokea jambo kama hilo nilihisi ni kitu kikubwa sana kilichonitokea maishani mwangu ".

Wakati Umutoni akijiandaa na siku ya kukutana na ndugu wengine waliozaliwa tumbo moja na mama yake na baba yake, sawa ameweza kufahamiana na mashangazi zake, mama yake mdogo na baadhi ya mabinamu zake, waliokua wanaoishi Rwanda na nje ya Rwanda .