Departing Dragon
Maelezo ya picha,

Chombo hicho kikipita juu ya anga la Johannesburg, Afrika Kusini

Wanaanga wa Marekani Doug Hurley na Bob Behnken wamekiondoa chombo chao ndani ya mtambo wa kuondokea kutoka kituo cha anga za mbali kwa ajili ya kuanza safari yao ya kurejea duniani.

Wawili hao wanatawajiwa kutua ndani ya maji kwenye eneo la mwambao wa Florida nchini Marekani muda mfupi baada ya saa nane za dakika aroibaini na tano 14:45 kwa saa za Marekani leo Jumapili.

Kutua salama kwa chombo hicho kutamaanisha kwamba Marekani kwa mara nyingine tena ina uwezo wa kuhudumu, ina kibali kamili cha watu wake kuweza kuingia katika uzio wa dunia na anga za mbali na kurejea duniani.

Uwezo huu ulipotea wakati nchi hiyo ilipoacha kutumia vyombo vyake vya safari za anga za mbali mwaka 2011.

Bob Behnken (L) and Doug Hurley (R)
Maelezo ya picha,

Bob Behnken (kushoto) na Doug Hurley (kulia) walianza safari yao ya kwenda kwenye kituo cha anga za mbali mwishoni mwa mwezi Mei

Shirika la safari za anga za mbali la Marekani Nasa na washirika wake wa kibiashara, SpaceX, wamechagua eneo chombo hicho kitakapotua mbali na eneo la kimbunga Isaias, ambacho kinaonekana ni kama kinaweza kupiga maeneo ya mwambao wa Florida.

Vyombo vingine vya uokozi kwa hiyo vinaongozwa kuelekea maeneo ya ghuba ya Mexico, kwenye eneo labahari la mwambao wa Pensacola magharibi mwa Florida.

Waongozaji wa safari ya chombo hicho wanafuata miongozo ipasavyo juu ya upepo unaohitajika wakati wa kutua na hali za mawimbi, na watachunguza utabiri wa hivi karibuni wa hali ya hewa kabla ya kuruhusu chombo hicho kutua.

Chombo hicho hushuka kwa kasi kubwa kinapotua, ambapo kinakadiriwa kuwa husafiri kilomita kadhaa kwa sekunde moja, na watashuhudia kikipata joto la takriban nyuzi joto 2,000 katika sehemu yake ya chini kitakapokua kikishuka chini na kupitia katika anga zenye hali ya hewa tofauti.

Wanaanga wa Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) Doug Hurley na Bob Behnken waliweka hitoria mwezi Mei walipoondoka katika kituo kilichopo pwani ya Florida.

Wawili hao walikwenda katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za mbali watatumia chombo kipya cha kampuni binafsi ya SpaceX.

Kawaida shirika la Nasa huwa linaendesha shughuli zake lenyewe katika anga lake.

Astronauts
Maelezo ya picha,

Doug Hurley (kushoto) na Bob Behnken (kulia) wamewahi kwenda kwenye anga za juu mara mbili

Lakini mara ya mwisho kwa Nasa kujitegemea kwa kila kitu ilikuwa mwaka 2011 ilipoendesha safari yake ya mwisho kwa kutumia chombo chake kwa jina space shuttle.

Shirika hilo sasa linataka safari zote za siku za usoni za kuzunguka dunia kuendeshwa kibiashara.

Na likiwa na matarajio kwamba safari ya Jumatato itakwenda vizuri, mfumo huu mpya wa kufanyakazi utaanza kutekelezwa kikamilifu.

"Sasa tunaanza mwanzo mpya wa safari za anga la juu; ni enzi ambayo anga ya juu itakuwa inafikiwa na watu wengi zaidi kuliko awali," ameelezea mkuu wa shirika la Nasa Jim Bridenstine.

"Tunatazamia siku za usoni ambapo safari za mzunguko wa dunia litakuwa suala la kibiashara kabisa, ambapo Nasa ni moja ya mteja kati ya wateja wengi na ambapo kuna watoa huduma wengi wanaoshindana kwa gharama, ubunifu na usalama."

Splashdown
Maelezo ya picha,

Nasa na SpaceX wakifanya mazoezi juu ya utaratibu wa kutua majini kwa chombo cha anga za mbali katka chombo kisichokua na watu mwaka jana

Mageuzi ya mavazi katika anga za mbali ni yapi?

Behnken (L) and Hurley

Mavazi yatakatovaliwa na wataalamu wa anga za mbali mwishoni mwa juma wakati chombo cha anga za mbali cha shirika la safari za anga za mbali la Marekani kitakapozindua safari ya chombo chake kinachoitwa Nasa Space X yamekuwa yakizungumziwa sana . Je yana utofauti gani na mavazi mengine yaliyovaliwa na wataalamu wa anga za mbali katika miaka mingine iliyopita?

Mavazi ambayo yanatajwa kuwa ni ya wakati ujao ambayo yatavaliwa na wanaanga Doug Hurley na Bob Behnken mwishoni mwa juma yanaonekana kuwa tofauti sana na yalke ya rangi ya manjano yaliyiovaliwa katika chombo kingine mara ya mwisho wakati wanaanga walipoanza safari yao kutoka kituo safari za anga za mbali cha -Kennedy Space Center.

Kofia zao za helmeti zimewekwa mfumo wa 3D- na glove zake mvaaji anaweza kuandika ama kufanya mabadiliko yoyote kwenye mitambo kwani zimetengenezwa kwa matumizi ya skrini.

Mavazi hayo -The Starman suits, kama yalivyoitwa, yote yapo pamoja na yametengenezwa ka ajili ya wanaanga. Muonekano wake ulibuniwa na mbunifu wa mavazi wa Hollywood Jose Fernandez, ambaye amefanyia kazi filamu za Captain America: Civil War na Batman v Superman: Dawn of Justice.

Lakini mavazi hayo yamebuniwa kwa ajili ya matumizi ya kuvaliwa ndani ya SpaceX , kifaa kinachofahamika kama Crew Dragon. Hayafai kutumiwa kwa matembezi ya anga za mbali.

Kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya anga za mbali ya Boeing pia ina mkataba na NASA kujaribu kuwabeba wanaanga katika kituo cha anga za mbali kwa ndege yake ya anga- CST-100 Starliner spacecraft. Pia imeweza kutengeneza kitengo cha hewa kwa ajili ya kuwalinda wanaanga katika nyakati muhimu za kuondoka na kuingia tena ndani ya chombo.

Bob Behnken and Doug Hurley
Maelezo ya picha,

Vazi la Bob Behnken alilolipeleka katika anga za mbali

Lakini lengo lake la msingi limesalia kuwa lile lile-kuwakinga wanaanga waliomo ndani yake dhidi ya hewa inayotoka ndani ya chombo, wakati inapotoka kwenye kifaa cha kutunza hewa. Pia hutoa hakikisho kwa wanaanga la kupata hewa safi ya oksijeni nay a kutosha na kudhibiti kiwango cha joto ndani ya chombo. Mawasiliano na waongozaji walioko ardhini hutolewa kupitia kofia ya helmeti.

Boeing Blue space suit
Maelezo ya picha,

Vazi la Boeing Blue, kama lilivyo valiwa na mwanaanga wa Nasa Chris Ferguson

Vazi jingine linaitwa Exploration Extravehicular Mobility Unit (xEMU) ambalo limetengenezwa ili kuvaliwa kwenye sakafu ya mwezi. Ni zito zaidi kuliko mavazi yaliyoundwa kwa ajili ya kuingiza hewa yaliyotengenezwa kwa ajili ya kuvaliwa ndani ya chombo chenyewe cha anga za mbali.

Hii ni kwasababu vazi hili linapaswa kumkinga mvaaji dhidi ya viwango vya hali ya juu vya joto nje ya ukuta wa chombo cha anga za mbali, na kumpatia kinga dhidi ya viumbe hai wa anga za mbali pamoja na chembechembe ndogo za vifusi vya angani. Kwa hilo, vazi hili linafanana na vazi la awali lililotumiwa kwa ajili ya matembezi katika kituo cha kimataifa cha anga za mbali( International Space Station)

Exploration Extravehicular Mobility Unit (xEMU) on the left and the Orion Crew Survival Suit
Maelezo ya picha,

Vazi la uvumbuzi au xEMU, (Kushoto) na vazi la kujinusuru angani yakionyeshwa katika maonyesho ya mwaka 2019

Kuna aina mbili za mavazi zilizotumiwa kwa ajili ya kutembea katika kituo cha Kimataifa cha safari za anga za mbali( ISS). Vazi moja lilikuwa ni la Kirusi aina ya Orlan, ambalo kwa mara ya kwanza lilitumiwa mwezi Disemba 1977.

Orlan ni vazi moja la anga .Likifahamika kama "backpack" linalofunguliwa kama mlango wa friji, na kumruhusu anayetembea katika anga za mbali kupanda ndani yake.

Vazi la Nasa la Extravehicular Mobility Suit (EMU) lilianzishwa mwaka 1981 na ni vazi la zamani zaidi ambalo limewahi kutumiwa kwa ajili ya matembezi ya anga za mbali katika kituo cha ISS.

PICHA

Cosmonaut Alexander Skvortsov outside the space station in 2014
Maelezo ya picha,

Cosmonaut Alexander Skvortsov akiwa amevalia vazi hili nje ya kituo cha anga za mbali mwaka 2014

Tofauti na Orlan, vazi la EMU linakuja kwa muundo wa vipande viwili tofauti-nusu ya chini na ya juu . Vazi hilo ambalo limekakamaa kiasi humuwezesha mtumiaji kulivaa kwa saa 8.5 nje ya hewa utupu ya anga za mbali.

Wanaanga watasafiri kwa treni ya kituo cha kimataifa cha anga za mbali (ISS) kwa mavazi yote mawili lile la EMU na Orlan.

Mavazi hayo yalivaliwa na wanaanga wa Apollo katika mwezi pia yaliitwa EMU. Yalikua ni matokeo ya miaka ya maendeleo.

Christer Fuglesang
Maelezo ya picha,

Mwanaanga Mswisi Christer Fuglesangakitembea katika anga za mbali katika EMU

Mavazi ya anga za anga za mbali yameanzia mbali tangu vazi la kwanza la kutembele katika anga za mbali lililovaliwa na marehemu Alexei Leonov Machi 1965.

Vazi la Leonov lilijaa hewa baada ya kutoka nje ya chombo na kuingia eneo la anga za mbali tupu,kwa hiyo mikono yake ikatoka nje ya glovu.

Ni kwa kutoka hewa tu nje ya vazi lake ,jambo lililomuweka katika hatari ya kuelea Mwanaanga huyo aliweza kurudi ndani ya chombo cha anga na kunusurika