AZAM FC imeziundia mikakati mizito timu za Simba na Yanga ili kuweza kuendelea kushikilia usukani wa ligi kwa kuhakikisha inafanikiwa kuibuka na pointi tatu katika kila mechi.

 

Azam FC inaongoza msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi nne, huku ikishinda michezo yote na kukusanya pointi 12, ambapo Simba inayoifuata ikiwa na pointi 10 na Yanga ina pointi 10 pia zikiwa zimetofautiana katika idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zacharia ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa, Azam imejipanga kuhakikisha inafanikiwa kushinda michezo yao yote ili kuendelea kubaki.

“Azam msimu huu tumejipanga kuhakikisha tunachukua kombe, tumeshajua mapungufu ambayo yalikuwa yakijitokeza katika baadhi ya mechi zetu hasa zile za mikoani ambapo wachezaji wamekuwa wakifanya mazoezi katika viwanja viwili tofauti cha nyasi bandia na cha vumbi.

 

“Tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu katika kila mechi tutakayocheza naikitokea iwapo tumepoteza ni kwa bahati mbaya, lakini tunahitaji ushindi mnono, mwalimu anatumia muda wake vyema kukipanga kikosi chake,” alisema Zaka Zakazi.