MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Babati mkoani Manyara katika Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa leo Jumapili Oktoba 25, 2020.

Rais Magufuli akiwa kwenye mkutano wa kampeni Babati amempigia simu Waziri wa Nishati na Madini, Meldard Kalemani kujua shida iliyosababisha Wananchi hao kukosa umeme na amempa mwezi mmoja kwa wateja hao waliolipa kuunganishiwa umeme.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Rehema Mashinji amesema wateja 4,000 wanaotaka Umeme Mkoa wa Manyara walishindwa kuunganishiwa umeme kutokana na changamoto ya fedha waliyonayo TANESCO mkoani hapo

Wateja hao waliolipia walishindwa kuunganishiwa umeme kwa kuwa pia wanahitaji nguzo za kuweza kufikishiwa umeme katika maeneo yao wanayotaka nishati ya umeme

Katika hatua nyingine Rais Dk. Magufuli amemuagiza Waziri Kalemani kuhakikisha analeta wataalamu wa Tanesco kuanzia kesho Jumatatu Oktoba 26, 2020 kuhakikisha wanakamilisha uunganishaji wa umeme kwa wananchi 400 ambao wamelipia kuunganishiwa umeme katika wilaya ya Babati lakini bado hawajaunganishwa.

 

Pia Dk. Magufuli amewapongeza wananchi wa Babati kwa kumpitisha bila kupigwa mbunge mteule wa jimbo hilo Pauline Gekur ambaye awali alikuwa ni mbunge wa CHADEMA.