Tume ya uchaguzi Zanzibar imemtangaza Dkt Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa urais Zanzibar.
Mgombea wa chama tawala cha CCM Hussein Mwinyi atangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27% huku mpinzani wake Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.87%.
Baada ya kutangazwa mshindi Dkt.Mwinyi amesema "Nimepokea ushindi kwa mikono miwili, Nashukuru kuwa wananchi walio wengi wamenichagua mimi na chama changu cha Mapinduzi kwa miaka mitano ijayo.
Nawashukuru kwa uvumilivu na ustahamilivu mkuwa. Niwashukuru zaidi kwa kunipigia kura za kutosheleza kuwa rasi wa Zanzibar. Nitalipa imani hii kwa utumishi uliotukuka," Dkt Mwinyi amesema.
Dkt.Mwinyi aliongeza kusema Zanzibar mpya itajengwa na Wazanzibari wote bila kujali itikadi , Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofuati zao.
"Mimi Hussein Mwinyi si bora kuliko CCM ushindi huu ni wa wana Wazanzibari wote ,uchaguzi sasa umekwisha turudi kujenga Zanzibar mpya.
Aidha amesisitiza wafuasi wa CCM ,washeherekee kwa ustaha bila kukwaza wengine kwa kuwa ushindi wasingepata pasipo kuwa na ushindani.
Ushindi huu umetangazwa wakati Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye ni mgombea wa urais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Seif Sharif Hamad akiwa amekamatwa kwa mara pili.
Maalim Seif alikamatwa muda mfupi baada ya kutangaza kuongoza maandamano ya amani ili kutetea haki yao ya kidemokrasia.
Siku ya Jumanne Maalim Seif alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha mtoni Garagara na na kupelekwa makao makuu ya polisi kisiwani Zanzibar ambako aliachiliwa saa kadhaa baadaye katika hatua ambayo ilishutumiwa vikali na viongozi wa upinzani.
0 Comments