Rais mteule John Pombe Magufuli amekabidhiwa cheti kwa ushindi wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu pia nae amekabidhiwa cheti ushindi cha Makamu Rais.

Jaji mstaafu na mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Semistocles Kaijage ndiye anayeongoza sherehe hizo baada ya chama tawala cha Mapinduzi kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28.