Nilipokutana na Ahmed, alikuwa peke yake ndani ya chumba. Alikuwa na alama mwilini mwake kutokana na kuchapo alichokuwa amepewa. Hajui ana miaka mingapi, lakini huenda ana umri wa miaka 10.
Shule anayosomea ni moja ya taasisi 23 ya mafunzo ya Kiislamu nchini, ambazo zinajulikana kama khalwas, ambayo nilinasa kanda ya video kisiri katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2018.
Nilishuhudia na kunasa kanda za video za watoto wengi, baadhi yao wana umri wa miaka mitano, ambao wanapigwa vibaya, kufungwa minyororo mara kwa mara na kufungiwa bila kupewa chakula au maji na masheikh wanaosimamia shule hizo. baadhi ya watoto ambao sikuwaangazia katika taarifa hii waliniambia walinajisiwa na kufanyiwa dhulma zingine za kingono.
Kuna karibu taasisi 30,000 za khalwas katika maeneo tofauti nchini, kwa mujibu wa serikali ya Sudan. Zinapokea fedha kutoka kwa serikali na misaada kutoka kwa wahisani ndani na nje ya nchi.
Watoto wanafunzwa kuhifadhi Quran. Kwasababu hazitozi ada yoyote, familia nchingi zinachukulia shule hizo kuwa elimu mbadala ya umma, haswa katika maeneo ya vijijini ambayo hakuna shule zinazoendeshwa na serikali. Wanafunzi huishi huko na kurudi nyumbani wakati wa likizo.
Kwa wengi shule hizo ambazo zimekuwa zikuhudumu kwa miaka na mikaka ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Wasudan, na huchukuliwa kama sehemu ya utambulisho wa kitaifa.
Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni video zinazoonesha watoto wakipigwa katika shule hizo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii, huku taarifa masheikh wanaotuhumiwa kuwabaka wanafunzi ndani ya khalwas zikiangaziwa katika vyombo vya habari nchini Sudan. Lakini Mashirika ya kutetea haki za binadamu zimepuuza madai hayo.
Nilitaka kufichua jinsi unyanyasaji unavyofanyika ndani ya shule hizi, na kuwapa sauti watoto ambao hawana nafasi ya kuelezea kile wanachopitia.
Mimi binafsi nilikabiliwa na hali wanayopita. Nikiwa kijana mdogo, Nilijiunga na khalwa. Kila siku nilikuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu kuepuka kichapo cha waalimu.
Nilijua kuwa nitakosana na marafiki na familia yangu kuhusiana na uchunguzi huu, lakini taarifa hii inastahili kuangaziwa. Nilituhumiwa kuwa sehemu ya "Njama ya magharibi kushambulio elimu ya kidini" na baadhi ya watu miliozungumza nao.
Kufikia wakati niliwasiliana na BBC, Nilikuwa nimenasakisiri kanda za video kwa miezi kadhaa. Katika khalwas ya kwanza niliyozuru ilikuwa inafahamika kama Haj el-Daly, ambako nilisikia watoto wanateswa. Niliingia katika shule hiyo kupitia msikitini na kuswali na wa watu wengine wakati wa sala ya mchana, na kuchukua video kwa kutomia simu yangu wakati nikiendelea na sala.
Nilipopiga magoti nilisikia sauti yakusikitisha. Nilipoangalia juu niliona watoto waliokuwa mbele yangu walikuwa wamefungwa nyororo miguuni kwa pamoja kama wanyama.
Maombi yalipoisha watoto hao walitoka msikitini na kuelekea upande mwingine. Lakini nilipokuwa natoka nilisikia makelele na sauti ya kilio.
Nilifuatilia sauti hiyo na kufika katika chumba kilichokuwa namwangaza mdogo, ambako nilimpata mtoto akilia, miguu yake ilikuwa imefungwa pamoja kwa minyororo. Nilianza kurekodi video ya kile nilichokiona. Huyu alikuwa Ahmed. Aliniambia anataka kwenda nyumbani. Nilijaribu kumtuliza lakini nilisikia sauti ya sheikh akizungumza kuja mahali tulipokuwa, niliacha kurekodi video na kuondoka katika khalwa hiyo.
Lakini nilirejea siku ya pili ili niweze kufichua mengi zaidi kuhusu vitendo ya ukatili vinavyofanywa dhidi ya watoto. Nilipokuwa nakizungumza na watoto na kurekodi video kwa kutumia simu yangu, Niligundua mmoja wa wanafunzi wakubwa kidogo alikuwa akiangalia nilichokuwa nikifanya. Aliondoka ghafla na baadaye alirejea akiwa na sheikhe anayesimamia shule hiyo.
Sheikh alianza kunikaripia na kuuliza, kwanini narekodi video ya wanafunzi. Nilifanikiwa kutoroka na kuingia mtaani.
Mamlaka ya usimamizi wa Haj el-Daly imeambia BBCkuwa kuna sheikh mpya anayesimamia shule hiyo na kuongeza kuwa visa vya watorto kupigwa na kufungwa minyororo miguuni vimekomeshwa.
Kumbukumbu yangu binfasi ya khalwa
Nilifika nyumbani nikiwa na uoga - laiti ningelishikwa hakuna mtu angelijua niko wapi. Lakini nilisikitishwasana na kile nilichokiona. Hali hiyo ilinikumbusha wakati wangu nilipokuwa khalwa kama mvulana mdogo, mahali ambapo kupigwa ni jambo la kawaida, japo hakuna mtu aliyefungwa minyororo miguuni.
Siku yangu ya kwanza kujiunga na khalwa nilikuwa na furaha sana wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 14, nikijipimisha sare zangu zinazofahamika kama jalabiya - nguo za kitamaduni - nikisubiri kwa hamu asubuhi ifike. Lakini awali niligundua kulikuwa na kitu ambacho sio cha kawaida, nilihisi kuna kitu ambacho sio cha sawa. Niligundua watoto walionekana kuwaogopa masheikhe mawaalimu.
Unyanyasaji ulianza nyakati za jioni. Tukiwa na usingizi au kufunga macho, sheikh alikuwa akituchapa. Hali ambayo bila shaka ilitufanya kuamka. Nilikaa katika khalwa kwa karibu mwezi mmoja, nikivumilia kuchapwa mara kwa mara. Niliporudi nyumbani, Niliwaambia wazazi wangu kuwa sitaki kurudi, japo sikuwaambia jinsi nilivyonyanyaswa. Hawakufurahia hatua yangu ya kutaka kuacha masomo, lakini hawakunilazimisha kurudi.
Baada ya kukaripiwa na sheikh anayesimamia chuo cha Haj el-Daly, nillikosa ujasiri wa kuendelea mbele na kurekodi video za unyanyasaji ndani ya khalwas. Niliwasilisha ushahidi wangu kwa waandishi waarabu wa habari za ufichuzi (ARIJ), ambao waliniunganisha na BBC idhaa wa Kiarabu. Kuanzia wakati huo mambo yalibadilika .
Mhariri wangu mjini London aliniunganisha na mtayarishi, Mamdouh Akbik. Yeye ni Msyria na mimi Msudan, japo sote tunazungumza kiarabu lafudhi zetu ni tofauti sana. Lakini baada ya muda tuliweza kufanya kazi pamoja vizuri sana
Tulichora ramani ya mahali zilipo khalwas, tukakusanya ushahidi, na kuzungumza juu ya usalama na vifaa kote. Lakini kilichobadilisha mambo ni wakati nilipokea vifaa vya kurekodi vya siri. Ilinipa ujasiri wa kuendelea na kazi yangu.
Sudan nchi kubwa iliyo na milima ,Bahari nyekundu na majangwa. Katika kipindi cha uchunguzi, huenda nilisafiri maili 3,000, hususana kwa basi.
Nilikutana na familia ambazo watoto wao wavulana walinyanyaswa vibaya. Katika baadhi ya visa wengine walifariki wakiwa shuleni na ilikuwa vigumu kubaini chanzo cha kifo.
Mashekhe wana ushawishi mkubwa katika jamii zao na ni nadra sana familia kuwasilisha kesi dhidi yao. Kesi zinazowasilishwa mahakamani zinajivuta hadi familia zinakufa moyo na kuachana nazo. Au wakati mwingine zinaishi kutatuliwa nje ya mahakama na familia kulipwa kulipwa fidia.
Baadhi ya familia zinaamini mashekhe hawana nia mbaya na kwamba lengo lao nikuwakuza wanafunzi katika maadili ya kidini, na ikiwa "ajali" ikitokea katika mchakato huo, basi ni amri ya Mungu.
Familia yangu yenyewe inakubaliana na nadharia hiyo. Hali iliyonibidi kufanya siri uchgunguzi wangu. Ilikuwa vigumu sana hasa wakati nilitembelea khalwa zilizopo nyumbani kwetu Kaskazini mw Darfur, ambako jamaa zetu wengi wanaishi.
Baada ya filamu hiyo kupeperushwa hewani, Nilifurushwa katika kundi la WhatsApp la familia. Nilidhani pengine wangeliniuliza maswali au kujadiliana na mimi, lakini badala yake nilitengwa. Lakini nilipigiwa simu na wazazi wangu ambao waliniambia wataniunga mkono japo walihofia sana usalama wangu. Nilishukuru sana wazazi wangu walinielewa.
0 Comments