Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 , kamanda wa anga za mbali amekuwa maarufu sana katika mitandao ya kijamii nchini Uchina kwa kazi yake ya mpango wa uvumbuzi wa mwezini wa chombo cha Chang'e-5.
Licha ya kuwa kamanda mwenye umri mdogo zaidi katika kituo cha safari za anga za mbali cha Wenchang Zhou Chengyu anafahamika kwa kazi yake kama Dada Mkubwa "Big Sister" kama ishara ya heshima kwake.
Safari ya chombo cha Chang'e-5 ndi safari ya tatu iliyokuwa ya mafanikio nchini Uchina ambapo chombo hicho kiliweza kutua mwezini baada ya miaka saba.
Bi Zhou alikuwa msimamizi wa mfumo wa kuunganisha roketi.
Mtaalamu huyo wa anga za mbali amekuwa akizungumziwa katika mtandao wa kijamii wa Uchina Weibo tangu alipoangaziwa na vyombo vya habari vya taifa la Uchina kama mmoja wa wanawake waliohusika katika kufanikisha safari ya chombo cha anga za mbali cha kichina - Chang'e-5 lunar tarehe 23 Novemba.
Taarifa yake ilipendwa sana na umma kutokana hasa na umri wake mdogo. Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakimpongeza kama mtu mwenye "kipaji cha kipekee na akili " na kumuelezea kama "mtu wa kujivuniwa " na taifa.
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Watu kadhaa wamekuwa wakifanya mzaha kwa kulinganisha mafanikio yake na yao, wakielezea ni kwa jinsi gani walivyoi nyuma yake kimaisha iwapo wangelinganishwa na yeye.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Duocai Guizhou Net, Bi Zhou amekataa mara kwa mara kufanya mahojiano kwasababu hataki umaarufu umpotezee muda wa kazi yake.
Lengo la safari ya chombo cha Chang'e-5 - ambacho kilipewa jina la muungu mwanamke wa Kichina- ni kukusanya miamba ya mwezini na udongo ili kusaidia wanasayansi kujifunza zaidi muundo wa mwezi.
Kama kitafanikiwa, itakuwa ni mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya 540 kuwezekana kuletwa kwa udongo na mawe kutoka mwezini duniani, na itaifanya China kuwa nchi ya tatu kufanya hivyo baada ya Marekani na Muungano wa Usovieti.
Mpango huo ni sehemu ya msukumo wa Beijing wa kutaka kuwa taifa lenye nguvu zaidi katika anga za mbali , huku vyombo vya habari kwa kitaifa vya Uchina vikitangaza moja kwa moja kile vinachoita "ndoto ya anga za mbali " - huku Rais Xi Jinping akiuita -hartua moja kuelekea "kulipatia taifa nguvu mpya''.
Kwa Uchina, uvumbuzi wa anga za mbali unaonekana kama njia ya kuonesha ukuaji wake wa uwezo wa kiteknolojia, pamoja na kujionesha kama msukumo wa kutambuliwa katika jukwa la dunia
Uchina imekuwa ikitaka kuonesha sana wanawake wenye uwezo mkubwa nchini humo katika miezi ya hivi karibuni. Uongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo umetawaliwa na wanaume kwa kiasi kikubwa , lakini mwezi Novemba , gazeti la taifa Global Times liliwaalika raia katika mitandao ya kijamii kutoa maoani yao kuhusu mafanikio ya mwaka ya wanawake kama vile mwanasayansi Chen Wei, msemaji wa wizara ya mambo ya nje mwanamke- Hua Chunying, na mpiganaji wa UFC mwanamke Zhang Weili.
Lakini wengi nchini China wanahisi nafasi ya wanawake nchini humo bado haionekani katika viwanda vingi. jambo hili lilizungumziwa sana mwezi Septemba, wakati wa kipindi cha maigizo cha TV kilichoonesha nafasi ya wanawake wa China katika mapambano dhidi ya Covid -19 kilipoonekana kama ubaguzi wa jinsia.
0 Comments