WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo ameamuru kukamatwa na kuwekwa ndani kwa viongozi na wasimamizi wa miradi ya Wakala wa Majengo nchini (TBA) kwa kuchukua kiasi kikubwa cha fedha wakati miradi iliyotolewa fedha utekelezaji wake umekwama.

 

TBA inadaiwa  ilichukua kiasi cha Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza miaka mitano iliyopita lakini hadi sasa nyumba hiyo imefikia usawa wa msingi.

 

Waziri Jafo pia alionesha kukerwa kutokana na kukwama kwa jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Uvinza ambapo kiasi cha Sh  milioni 900 kimetolewa lakini mradi umekwama kwa miaka zaidi ya mitatu na sasa ujenzi upo usawa wa madirisha.