Kituo kimoja cha redio nchini Kenya kimetozwa faini ya kiasi cha shilingi milioni moja sawa na dola za Marekani 9,000 baada ya wafanyakazi watatu wa kituo hicho kutumia ma redio kutoa lawama kwa waathirika wa vitendo vya ubakaji.
Watu hao watatu waliwalaumu wanawake kwa vitendo vilivyowapata, kutokana na kujirahisisha mno kwa wanaume. Hii ni faini ya kwanza kutolewa tangu wanawake nchini Kenya kutoa wito wa kuwekwa kwa kanuni za maudhui ya redio.
Kwa wiki tatu sasa, wanawake wa Kenya wamekuwa wakipeleka kilio chao kwenye mitandao ya kijamii wakidai haki kwa wanawake waliobakwa na kudhalilishwa kijinsia.
Wamekuwa wakielekeza hasira yao kwa wanaume wanaounga mkono unyanyasaji wa kijinsia na kuwakosoa waathirika wavitendo hivyo.
Chanzo kilikuwa shambulio la watangazaji wawili wa redio na DJ kuhusu mwanamke ambaye alikuwa amemkataa mwanaume na baadaye akasukumwa kutoka ghorofa ya 12 .
Mwanamke huyo mwenye miaka 20 sasa amekuwa mlemavu kutokana na tukio hilo.
Mshukiwa alikana mashtaka dhidi yake na sasa yuko nje kwa dhamana.
Kituo hicho cha redio kimewafukuza kazi wafanyakazi hao watatu.
0 Comments