MAOFISA wa magereza Kaunti ya Kakamega walikuwa na wakati mgumu kumtuliza mfungwa mmoja aliyekwea juu ya ukuta ya gereza hilo akitishia kujitoa uhai kwa madai ya kupewa chakula kidogo.

 

Mfungwa huyo, katika gereza la Kakamega anahudumia kifungo kwa makosa ya mauaji pamoja na wizi wa kimabavu.

 

Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Gereza hilo Japhet Onchiri, alisema mfungwa huyo alikwea juu ya ukuta huo lenye kimo cha mita 100 asubuhi ya Jumamosi akidinda kushuka hadi pale matakwa yake yatakaposikizwa.

 

Hatimaye mfungwa huyo anaripotiwa kushuka kutoka kwa ukuta huo baada ya kulemewa na miale mikali ya jua kwa kuwa hakuwa na nguo zozote.