Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo
Image caption: Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema kuwa vikosi vyake vimekabiliana na wenzao wa Rwanda karibu na mpaka wa mashariki siku ya Jumatatu.

Msemaji wa jeshi katika Mkoa wa Kivu Kaskazini alisema vikosi vya Rwanda vilivuka mpaka na kuingia Congo katika hatua ambayo ilisababisha makabiliano.

“Kitengo cha wanajeshi wa Rwanda kiliingia kilomita tano ndani ya Congo…Hauwezi kuelezea jinsi wanajeshi waliojihami walivuka mpaka na kuanza kupiga risasi," Brigedia Jeneral Sylvain Ekenge taliambia BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

Majeshi ya Rwanda hayajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo au kujibu ombi la BBC.

Ramani

Video zinazoshirikishwa mitandaoni zinawaonesha wenyeji waliokuwa na hofu wakikimbia huku vikosi hivyo viwili vikikabiliana kwa rasasi. Wanajeshi wa Rwanda baadaye walirudi nyuma na kwenda nyumbani.

“Kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyefariki katika tukio hilo”, Jenerali Ekenge alisema.

Viongozi na wakazi wa eneo hilo walirejea majumbani mwao baada ya hali ya utulivu kudumishwa.

Mvutano wa mipaka kati ya majirani hao wawili wa Afrika Mashariki ni jambo la kawaida kwa sababu ya biashara haramu, ukosefu wa mipaka wazi na mashambulio ya waasi.

Tshisekedi na Kagame watofautiana kuhusu 'ukatili DRC'

Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?