Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka askari Polisi kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kuvitendea haki vyeo vipya walivyovipata kwa kuhakikisha wanatimiza na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa katika kambi ya medani ya kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, wakati akifunga mafunzo ya Kozi ya Uongozi Mdogo Ngazi ya Cheo cha Koplo wa Polisi ambapo jumla ya askari 1697 wamehitimu mafunzo hayo na kutunukiwa Cheo hicho cha KOPLO.

Naye Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi SACP Ramadhan Mungi amesema shule hiyo ilipokea jumla ya wanafunzi 1712 na waliofanikiwa kuhitimu mafunzo hayo ni 1697 huku wengine 15 wakiachishwa mafunzo kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha amesema mafunzo waliyopatuiwa yatasaidia kuwaongezea weledina maadili  na kupandisha viwango vyao vya uadilifu, uwaminifu, utii haki na uzalendo pamoja na kudumisha ukakamavu, ujasiri na nidhamu katika utendaji wa kazi zao za kila siku.