Miongoni mwa matukio makubwa yaliyotokea nchini humo ni kuaga dunia kwa rais aliyekuwa madarakani hayati John Pombe Magufuli.

Tanzania ilijipata katika histori-kwanza kumpoteza kiongozi aliyekuwa madarakani na pili kumpata rais wa kwanza mwanamke .

Baadhi ya viongozi walizungumzia kuguswa na msiba huo huku makamau wa rais Samia Suluhu Hassan akiapishwa na kuendelea na kazi ya mtangulizi wake .

Mwanasiasa maarufu wa upinzani Sheikh Shariff Hamad pia aliaga dunia na kuitumbukiza Tanzania katika hali ya maombolezo.Mwaka wa 2021 pia ulikuwa mgumu kwa Tanzania kama nchi nyingi za dunia kwa sababu ya kukabiliana na janga la Corona.

Kifo cha Magufuli

Usiku wa tarehe 17 Jumatano Machi mwaka wa 2021 makamu wa rais wakati huo Samia Suluhu Hassa aliitangazia nchi na ulimwengu kuhusu kuaga dunia kwa rais wao Dkt.John Pombe Magufuli.Kilikuwa ni kifo ambacho kiliiacha nchi hiyo na simanzi huku rambi rambi zikianza kumiminika kutoka kwa viongozi kote nchini humo,kandaa hii na duniani.Mengi yaliendelea kufanyika na kikatiba,Samia kama makamu wa rais aliapishwa baadaye kuiongoza nchi kama rais .

Raia wa Tanzania walifunga baadhi barabara za jiji la Dar Es Salaam ,Zanzibar na maeneo mengine kwa shughuli ya kuuaga mwili wa Magufuli.Wengi waliguswa na msiba huo na kote kulikuwa na majonzi.

Kuapishwa kwa rais Samia Suluhu Hassan

Kutokana na uzito wa msiba huo pia watu wengi walianza kuwa na mashaka kuhusu kitakachofuata kuhusu uongozi wa Tanzania.Je,rais Samia itakuaje?wengi walizingumza akiwemo kuhusu mustabali wa hatua itakayofuata ya wa Samia kuchukua uongozi wa nchi kama inavyotakikana na katiba .Kwa wanaomfahamu rais Samia kama aliyekuwa rais wa Zanzibar na makamu wa rasi wa zamani wa Tanzania Dkt Mohammed Shein rais Sami ani mtu wa kuaminiwa kwani alisema;

‘Ni mtu ambaye anadhibiti siri na anayasema anayoyafanya hamkaripii asiyehusika’

Habari za msiba hazikukomea hapo kwa mwaka wa 2021 kwani kilitokea kifo cha aliyekuwa katibu mkuu kiongozi John Kijazi ,mwanasiasa maarufu wa upinzani Maalim Sheikh Shariff Hamad aliyekuwa makamu wa rais wa kwanza visiwani na Zanzibar ambaye kifo chake kilitangazwa na rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi

Kuendelea kupambana na Janga la Corona

Mwaka wa 2021 Tanzania iliendelea kupambana na janga la Corona kama nchi nyingi ulimwenguni.Nchi hiyo ilibadilisha sera na kuanza kuchukua hatua za kuzuia maambukizo ya ugonjwa huo Pamoja na kuchukua tahadhari.

Hatua nyingine muhimu katika mapambano yake dhidi ya virusi hivyo ni kukubaliwa kwa chanjo dhidi ya Uviko 19 ambapo tayari watu walianza kupokea chanjo baada yar ais Samia Suluhu Hassan kuongoza shughuli ya kuipokea chanjo .

Kukamatwa kwa kiongozi wa Upinzani Freeman mbowe

Katika upande wa masuala kisiasa mwaka 2021,kiongozi mkuu wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi.Ikiwa ni moja ya tukio ambalo ndani ya mwaka huo,limekuwa gumzo,huku kesi ikiendelea mahakamani.

Katika mkutano wake na viongozi wa vyama vya siasa,rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwafunda viongozi namna ambavyo wanatakiwa kuendesha shughuli zao za kisiasa.Pia alitimiza ahadi yake ya kukutana na vongozi wa vyama vya kisiasa nchini humo katika kinacholeta matumaini ya uwezekano wa ushirikiano na maridhiano ya kisiasa katika siku zijazo nchini humo.