Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Februari 24, 2022 imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

 

Madabida ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI) na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo ya kusambaza makopo 7, 776 ya dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antiretroviral, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na zimetengenezwa nchini.